Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 09:01

Utaratibu wa mazishi ya Malkia na kutangazwa rasmi Mfalme Charles III


Mfalme wa Uingereza Charles III akilihutubia taifa siku ya Ijumaa.
Mfalme wa Uingereza Charles III akilihutubia taifa siku ya Ijumaa.

Kasri ya Buckingham imesema kutakuwa na kipindi cha maombolezo cha wanafamilia na nyumbani kwa mfalme mpaka wiki moja baada ya mazishi, tarehe ambayo haijathibitishwa lakini inategemewa kutangazwa katika siku kumi zijazo.

Kengele za kanisani zilisikika kote Uingereza Ijumaa wakati Mfalme Charles III akijiandaa kuwahutubia raia wake wenye huzuni siku ya kwanza kamili ya utawala wake mpya kufuatia kifo cha mama yake, Malkia Elizabeth II.

Hivi ndivyo shughuli mbalimbali zimepangwa kufanyika:

Mfalme Charles III
Mfalme Charles III

Mfalme Charles III atahutubia taifa saa mbili usiku, saa za Afrika Mashariki (1700 GMT), Spika wa Bunge la Uingereza Lindsay Hoyle alisema Ijumaa baada ya mtawala mpya kuingia madarakani.

Mfalme Charles na mkewe waliondoka kutoka makazi ya Balmoral Castle huko Scotland Ijumaa mahali ambako mama yake, Malkia Elizabeth II, alifariki Alhamisi mchana. Mwili wake utabakia huko kwa muda mfupi kabla haujahamishwa mjini London.

Hoyle alisema kikao maalum cha Bunge, kimeitishwa kutoa heshima zao kwa Elizabeth II, kitasitishwa muda wa saa kumi na mbili jioni “ wakati Mfalme atakapo hotubia taifa.”

Bunge la Uingereza, London, March 2, 2022.
Bunge la Uingereza, London, March 2, 2022.

-Jumamosi, Septemba 10-

Siku ya kwanza: Mpango wa siku kumi baada ya kifo cha malkia unaanza na Baraza la Utawala kukutana ili Charles atangazwe rasmi ni mfalme.

Wapiga tarumbeta watatu watatangaza kutawazwa kwake kwa shangwe. Kutangazwa huko kutasomwa kutoka katika roshani ya Kasri ya Mtakatifu James mjini London, halafu nchi nzima.

Charles atakuwa na mikutano na wananchi, vyombo vya habari vitapewa muhtasari wa mazungumzo yake kupitia afisa mwandamizi wa ofisi ya Mfalme anayehusika na kutawazwa kwa mfalme na mazishi ya kiserikali ya malkia, katika siku sijazo.

-Jumapili, Septemba 11-
Siku ya pili: Jeneza la Malkia linatarajiwa kusafirishwa kutoka Balmoral kwenda katika Kasri ya Holyroodhouse, makazi yake malkia rasmi mjini Edinburgh huko Scotland.

Safari hiyo kwa njia ya barabara itapita katika miji mingi midogo na vijiji, kuwapa fursa wananchi wa Uingereza nafasi yao kwanza kutoa heshima zao.

Preparations for the queen's death in Scotland are codenamed "Operation Unicorn" after the country's national animal.

Matayarisho kwa ajili ya maziko ya malkia huko Scotland yamepewa jina maalum “Operesheni Unicorn” likiwa jina la mnyama wa kitaifa.

-Jumatatu, Septemba 12-

Siku ya tatu: Charles anatarajiwa kuanza ziara ya England, Scotland, Wales na Ireland Kaskazini, nchi nne zinazounda Uingereza katika operesheni iliyopewa jina maalum “Spring Tide”.

Ramani ya UK.
Ramani ya UK.

Jeneza la malkia linatarajiwa kupelekwa kwa gwaride hadi Royal Mile huko Edinburgh kutoka Holyrood hadi kanisa la Mtakatifu Giles, ambako kutakuwa na ibada na maombi yatakayohudhuriwa na wanafamilia.

-Jumanne, Septemba 13

Siku ya Nne: Jeneza linatarajiwa kusafirishwa kwa ndege hadi mji mkuu na kupelekwa kwa njia ya barabara hadi Kasri ya Buckingham mjini London.

Watu wote wanatarajiwa kujipanga barabarani ambako jeneza hilo litapita.

Mtoto anaweka maua kwenye bustani ya Kasri ya Holyroodhouse huko Edinburgh, Scotland, on Sept. 8, 2022, baada ya kutangazwa kifo cha Malkia Elizabeth II.
Mtoto anaweka maua kwenye bustani ya Kasri ya Holyroodhouse huko Edinburgh, Scotland, on Sept. 8, 2022, baada ya kutangazwa kifo cha Malkia Elizabeth II.

-Jumatano, Septemba 14-

Siku ya tano: Gwaride la heshima kwa ajili ya jeneza hilo kupitia London linatarajiwa kufanyika, likifuatiwa na kuwekwa mwili kitaifa, katika Ukumbi wa Westminster wa Bunge, uliopewa jina maalum “Operesheni Feather”.

Wakuu wa familia ya kifalme wanatarajiwa kusimama kuzunguka jeneza hilo katika utamaduni unaojulikana kama Maombi ya Princes.

-Septemba 15-17-

Siku ya 6,7 na 8: Mwili utabakia katika ukumbi wa serikali. Wananchi wa Uingereza wanaweza kutoa heshima zao, kwa kupita mbele ya jeneza hilo liliyowekwa katika jukwaa lililopambwa kuadhimisha kifo cha mtu muhimu.

-Jumapili, Septemba 18-

Siku ya tisa: Mapokezi yatafanyika kwa viongozi wanaowasili na wakuu wa nchi ambao wamewasili kwa ajili ya maziko.

- Monday, September 19 –

-Monday, Septemba 19-

Siku ya 10: Maziko ya kitaifa yanatarajiwa kufanyika huko Westminster Abbey na umati wa watu utakuwepo katikati ya London.

Wakuu wa familia ya kifalme wanaweza kuamua kutembea nyuma ya jeneza wakati likibebwa na toroli la bunduki hadi katika abbey huku kukiwa na kimya cha dakika mbili.

Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Rais wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kuwa kati ya viongozi wa dunia watakao hudhuria mazishi yake Malkia.

Baada ya hapo jeneza la malkia litapelekwa hadi Kasri ya Windsor kwa ajili ya matangazo ya ibada maalum ya kuiombea maiti katika Kanisa la Mtakatifu George.

Baada ya hapo atazikwa kwa faragha katika kanisa la kumbukumbu ya Mfalme George VI, pembeni ya kaburi la mumewe, Prince Philip, majivu ya dada yake Princes Margaret, mama yao, pia akiitwa Elizabeth, na baba George VI.

Repoti hii inatokana na taarifa za mashirika ya habari ya Reuters na AFP

XS
SM
MD
LG