Waziri Mkuu mpya wa Uingereza Liz Truss amechagua baraza la mawaziri ambapo kwa mara ya kwanza mzungu hatoshikilia moja ya nafasi nne muhimu za uwaziri nchini humo. Truss alimteua Kwasi Kwarteng ambaye wazazi wake walitokea Ghana katika miaka ya 1960 kama waziri wa kwanza wa fedha mweusi wa uingereza, wakati James Cleverly anakuwa waziri wa kwanza wa mambo ya nje mweusi.
Cleverly ambaye mama yake anatokea Sierra Leone na baba yake mzungu siku za nyuma alizungumzia kuhusu alivyokuwa akionewa kama mtoto wa rangi mchanganyiko na amesema chama hicho kinahitaji kufanya juhudi Zaidi kuwavutia wapiga kura weusi.
Suella Braverman ambaye wazazi wake walihamia uingereza kutoka Kenya na Mauritius miongo sita iliyopita, anachukua nafasi ya Priti Pater kama waziri wa pili wa mambo ya ndani.
Utofauti unaoongezeka kwa sehemu unatokana na msukumo wa chama cha Conservative katika miaka ya karibuni kuwaweka mbele wagombea mbalimbali wa ubunge.