Miongoni mwa viongozi waliotoa pole zao ni pamoja na waziri mkuu mpya wa Uingereza Liz Truss ambaye kupitia taarifa muda mfupi baada ya kifo hicho kutokea, aliandika kwamba "taifa lote limeshtushwa na tukio hilo", akiongeza kwamba, "Malkia alikuwa msingi imara ampapo Uingereza ya sasa imesimama".
Mkuu wa kamisheni ya Umoja wa Ulaya ,Ursula von der Leyen, katika ujumbe wake amesema kwamba, "Malkia Elizabeth wa pili alishuhudia vita pamoja na maridhiano, huku akiwa nguzo muhimu katika kuleta mabadilko katika jamii na ulimwengu kwa ujumla".
Rais wa Marekani Joe Biden kwa upande wake amesema kwamba Elizabeth alikuwa zaidi ya Malkia aliyetikisa kizazi. Biden pia ameamuru bendera ya Marekani kupeperushwa nusu mlingoti ndani na nje ya nchi kama kumbukumbu yake hadi pale atakapozikwa.