Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 10:03

Malkia Elizabeth afariki akiwa na umri wa miaka 96


Hayati Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza
Hayati Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza

Malkia Eizabeth wa Pili wa Uingereza aliaga dunia Alhamisi akiwa na umri wa miaka 96."Malkia aliaga dunia kwa amani alasiri hii," familia ya Kifalme ilitangaza kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii.

Mwanawe Charles, ambaye sasa ni Mfalme, atarejea London siku ya Ijumaa.

Awali, kasri ya Buckingham ilikuwa imetoa taarifa ikieleza wasiwasi juu ya afya ya Malkia huyo baada ya kufanyiwa tathmini ya afya yake Alhamisi.

Taarifa hiyo ilisema madaktari wa mfalme wa Uingereza walikuwa wamependekeza awekwe katika uangalizi wa kiafya.

Ilisema alikuwa katika nyumba yake ya Balmoral huko Scotland, makazi yake wakati wa majira ya joto.

Malkia alifuta mkutano wa Jumatano aliokuwa anakutana na Baraza la Privy, kikundi cha karibu yake, washauri wake wanaoaminika sana. BBC imeripoti Alhamisi kuwa Prince Charles na wanafamilia wengine wa ufalme huo wanasafiri kuelekea Balmoral ili wawe pamoja na Malkia.

Kutoka katika akaunti yake ya Twitter, Waziri Mkuu Liz Truss alisema “nchi nzima” ina “wasiwasi mkubwa” kwa habari hizo. Aliongeza kuwa, “Fikra zangu – na fikra za watu wote kote Uingereza – ziko pamoja na mtukufu Malkia na familia yake wakati huu.”

Malkia alimteua Truss kuwa waziri mkuu huko Balmoral Jumanne, badala ya kusafiri kwenda London kwa tukio hilo. Katika kipindi cha miaka 70 ya utawala wake Malkia amekuwa na kawaida ya kukutana na waziri mkuu mpya katika Kasri ya Buckingham.

XS
SM
MD
LG