Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 15:22

Waziri Mkuu Truss kuweka mipango ya kukabiliana na ongezeko la bili za umeme


Liz Truss alipowasili katika ofisi yake iliyoko mtaa wa Downing Street.
Liz Truss alipowasili katika ofisi yake iliyoko mtaa wa Downing Street.

Truss, aliteuliwa kuwa Waziri mkuu Jumanne, ameahidi kuchukua hatua mara moja kutatua moja ya changamoto kadhaa zilizo ngumu kabisa kwa kiongozi anayeingia madarakani katika historia ya kipindi baada ya vita ikiwemo kupanda kwa bili za umeme, kudorora kwa uchumi na migomo ya wafanyakazi viwandani.

Aliongoza mkutano wa baraza la mawaziri lake jipya Jumatano kabla ya kuzungumza kwa mara ya kwanza katika bunge kama kiongozi wa chama cha Consevative, akienda sambamba na kiongozi wa upinzani wa chama cha Labour Keir Starmer katika kujibu maswali yanayomhusu Waziri Mkuu.

“Napinga kuongeza kodi. Naamini ni makosa kuzikera kampuni zinazowekeza Uingereza,” Truss aliwaambia wabunge, akiongeza atatoa maelezo zaidi siku ya Alhamisi.

Chanzo cha habari kinachofahamu hali hiyo kimeliambia shirika la habari Reuters kuwa Truss alikuwa anafikiria kusitisha bili za umeme katika mpango ambao unaweza kuigharimu hadi dola bilioni 115.33, ikivuka kiwango kilicholipwa kwa waliolazimika kubaki nyumbani wakati wa COVID-19.

Waziri wa Fedha mpya Kwasi Kwarteng amewaambia viongozi wa biashara kuwa ukopaji utakuwa mkubwa katika kipindi kifupi ili kutoa msaada kwa kaya na biashara.

Wawekezaji wameelezea hofu yao ya kiwango cha ziada cha kukopa ambacho serikali pengine itahitaji kukitekeleza ili kufadhili mpango wake wa kusaidia na kupunguza kodi kuliko ahidiwa na Truss wakati wa kampeni yake ya uongozi.

Maafisa wa Benki ya Uingereza waliwaambia wabunge kwamba mipango ya Truss huenda ikasaidia kupunguza kasi ya Uingereza ya kuongezeka kwa mfumuko wa bei, lakini ilikuwa ni mapema mno kusema kutakuwa na athari kwa viwango vya riba.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

XS
SM
MD
LG