Shirika la habari la the Telegraph limeripoti kwamba chama cha Conservative kimelazimika kubadilisha mpangilio wa uchaguzi huo.
Kura za wapiga kura 160,000 zinazosafirishwa kwa njia ya posta zinatarajiwa kuwafikia Agosti 11.
Aliyekuwa Waziri wa Fedha Rishi Sunak, na Waziri wa Mambo ya Nje Liz Truss wanapigiwa upatu mkubwa wa kumrithi Boris Johnson kama Waziri Mkuu wa Uingereza.
Ukusanyaji wa maoni unaonyesha kwamba Truss ana ufuasi mkubwa akilinganishwa na Sunak.
Mshindi atajulikana Septemba tarehe 5.