Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 02:39

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson amejiuzulu


British Prime Minister Boris Johnson makes a statement at Downing Street in London, July 7, 2022.
British Prime Minister Boris Johnson makes a statement at Downing Street in London, July 7, 2022.

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson amejiuzulu kama kiongozi wa chama kinachotawala cha conservative lakini atasalia kuwa waziri mkuu hadi wakati kiongozi mpya atakapopatikana.

Tangazo hilo limatolewa Alhamisi baada ya mawaziri kadhaa na mawaziri wadogo zaidi ya 40, na washauri wao kujiuzulu katika nyadhifa zao, huku wakimtaka Johnson kuachia madaraka Jumatano jioni.

Hata hivyo Johnson alikuwa akikaidi, na kuapa kubakia mamlakani baada ya serikali yake kukabiliwa na kashfa kadhaa za kimaadili. Johnson alikuwa akijibu maswali magumu kutoka kwa wabunge, siku moja baada ya waziri wa fedha Rishi Sunak na mwenzake wa afya Sajid Javid kujiuzulu bila kutarajiwa, wakilalamikia ukosefu wa maadili kwenye utawala wake.

XS
SM
MD
LG