Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:19

Uingereza: Wagombea wanane wapambana kumrithi Boris Johnson


Mbunge wa chama cha Conservative Rishi Sunak akizundua kampeni yake kukiongoza chama na kuchukua nafasi ya waziri mkuu Boris Johnson, Julai 12, 2022. Picha ya AP
Mbunge wa chama cha Conservative Rishi Sunak akizundua kampeni yake kukiongoza chama na kuchukua nafasi ya waziri mkuu Boris Johnson, Julai 12, 2022. Picha ya AP

Wagombea wanane wa Conservatives watapambana kutaka kumrithi Boris Johnson kama kiongozi wa chama na waziri mkuu wa Uingereza baada ya kupata kura za kutosha kutoka kwa wanachama wenzao kupitia duru ya kwanza ya upigaji kura leo Jumatano.

Wagombea wawili pekee ndio walishindwa kupata uteuzi wa watu 20 wanaohitajika na hivo kuacha uwanja mpana wa wagombea wanaotaka kuungwa mkono na chama kwa ahadi za kupunguza kodi, uaminifu na serikali inayojali wanainchi, tofauti na Johnson ambaye alilazimika kutangaza kujiuzulu baada ya msururu wa kashfa.

Waziri wa zamani wa fedha Rishi Sunak anaungwa mkono na matajiri, miongoni mwa wanaowania nafasi ya waziri mkuu ni mrithi wake Nadhim Zahawi na waziri wa mambo ya nje Liz Truss katika mchuano unaozidi kuwa mkali na wenye mgawanyiko.

Kiongozi ajaye wa Uingereza anakabiliwa na hali ngumu huku uungwaji mkono kwa Maconservatives ukididimia pia, kura za maoni zimeonyesha.

Uchumi wa Uingereza unakabiliwa na mfumuko mkubwa wa bei, deni kubwa, na ukuaji mdogo wa uchumi huku watu wakilazimika kubana zaidi matumzi ya fedha zao katika miongo kadhaa. Haya yote yanatokana na upungufu wa nishati uliochochewa na vita vya Ukraine ambavyo vilisababisha bei ya mafuta kupanda.

XS
SM
MD
LG