Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 19:34

Liz Truss achukua wadhifa wa waziri mkuu mpya wa Uingereza


Waziri mkuu pya Uingereza Liz Truss akiwa Downing Street mjini London.
Waziri mkuu pya Uingereza Liz Truss akiwa Downing Street mjini London.

Liz Truss amechukua wadhifa wa waziri mkuu mpya wa Uingereza Jumanne, akichukua nafasi ya Boris Johnson wakati wa msukosuko wa kiuchumi na gharama  za nishati zinazoongezeka.

Johnson aliwasilisha rasmi kujiuzulu kwake kwa Malkia Elizabeth II katika eneo lake la Balmoral huko Scotland, ambapo malkia alimteua Truss kama waziri mkuu.

Truss mwenye umri wa miaka 47 anakuwa mwanamke wa tatu kuongoza nchi hiyo na waziri mkuu wa nne wa Uingereza katika kipindi cha miaka sita.

Alishinda katika kura ya ndani ya chama Jumatatu, akimshinda Waziri wa zamani wa Fedha Rishi Sunak.

Baada ya ushindi wake kutangazwa, Truss aliuambia mkutano wa chama, "Nilifanya kampeni kama M-Conservative, na nitatawala kama Mconservative.

XS
SM
MD
LG