Truss ameapa kuchukua hatua ndani ya wiki moja baada ya kuchaguliwa kushugulikia suala la kupanda kwa gharama za maisha kulikochochewa zaidi na kupanda kwa bei ya mafuta kufuatia mapigano ya Ukraine. Hata hivyo wakati akizungumza na shirika la habari la BBC Jumapili, hakueleza kwa kina kuhusu hatua anazokusudia kuchukua.
Licha ya kuteoeleza kwa kina mpango wake, Truss amesema kwamba anaelewa matatizo yanayoikumba Uingereza, miongoni wao yakiwa ni serikali kushindwa kushugulikia suala la kushuka kwa thamani ya sarafu yake, mazingira ya wafanyakazi pamoja na mfumo wa afya usio thabiti, tangu Julai baada ya waziri mkuu Boris Johnson kutangaza nia yake ya kujiuzu, suala lililopelekea kampeni kali za kutafuta mrithi wake.
Chama cha Konsavative kinatarajiwa kutangaza mshindi atakayechukua nafasi ya Jonhson Jumatatu. Truss anapambana na Rishi Sunak, waziri wa zamani wa fedha kuwania nafasiya waziri mkuu wakati atakayeibuka mshindi pia akifanyika mkuu wa chama hicho. Wakati wa kampeni, Truss aliahidi kuongeza matumizi ya fedha za ulinzi, kupunguza kodi pamoja na kuongeza nishati, ingawa hakueleza kwa kina anavyokusudia kutekeleza hayo.