Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 09:26

Tanzia ya Malkia Elizabeth II wa Uingereza


Malkia Elizabeth II
Malkia Elizabeth II

Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza amefariki akiwa na umri wa miaka 96 kwenye makazi yake huko Scotland.

Alikuwa ni kiongozi wa muda mrefu katika utawala wa kifalme duniani na mwaka huu alisherehekea miaka 70 ya kushikilia taji hilo.

Mwandishi Henry Ridgwell anaangalia maisha ya mmoja wa viongozi walioheshimiwa sana duniani.

Alikuwa kiongozi pekee wa kifalme ambao waingerea wanaishi leo wamewahi kuwafahamu, ni mfano taifa, himaya yake na jumuiya ya madola. Alionyesha nguvu ya Uingereza na tabia yake muda mrefu kabla hata ya kujua atakuwa malkia.

Malkia Elizabeth II alisema:“Natangaza mbele yenu nyote kuwa maisha yangu yote, yawe marefu au mafupi, nitajitolea kuwahudumia na kwa huduma kwa familia yangu kubwa ya kifalme ambayo sote ndiyo tuko humo.”

Akiwa na umri wa miaka 25, Elizabeth aliingia katika uongozi wa kifalme baada ya kifo cha baba yake George wa sita, takriban miaka mitano tu baada ya kuolewa na mzaliwa wa Ugiriki, Prince Phillip.

Alishuhudia mabadiliko makubwa na ya kina katika jamii na teknolojia wakati wa utawala wa zaidi ya miongo saba, wakati ambapo alionya kuhusu hatari za kutu kuachana na maadili ya zamani wakati wakikumbatia fursa za uvumbuzi mpya.

Aliandika tweet yake ya kwanza mwaka 2014. Kuna rekodi chache ambazo hakuzivunja: alikuwa ni kiongozi wa muda mrefu duniani katika himaya ya kifalme.

((Richard Fitzwilliams, Mwandishi na Mchambuzi wa Masuala ya Kifalme))
“Kama mkuu wa Jumuiya ya Madola, malkia ana uhusiano na matukio yaliyopita. Mara nyingine ilikuwa ni matukio magumu kwasababu dhana ya ufalme, wakiangalia unyanyasaji wa kikoloni na ufalme. Lakini malkia alikuwa na wasi wasi, nadhani kwasababu ya nia yake ya dhati kwa taasisi.”

Aliwakilisha urafiki wa Uingereza kwa wale ambao walikuwa na thamini sawa na za Uingereza kama vile uhuru, usawa, na demokrasia. Kwajeshima alikabiliana na wale waliokuwa na mtizamo tofauti.

Kuonekana naye ilikuwa na maana ya kupata fursa nzuri na heshima kubwa.

Malkia wa Uingereza Elizabeth
Malkia wa Uingereza Elizabeth

Malkia pia alikuwa akikosolewa katika nchi yake mwenyewe. Wa Marengo wa kushoto walimlenga kama mfano wa taasisi ambayo haiku sawa katika enzi hii ya sasa, uhuru mambo leo na demokrasia duniani na mzigo kwa mlipa kodi wa Uingereza.

Kifo cha Princess Diana ambaye alikuwa maarufu sana kilikuwa ni fursa nzuri kwa wakosoaji wake kumshutumu kwa kuwa kimya na kuchukua muda kuelezea chochote.

Princess Diana
Princess Diana

Malkia Elizabeth II alieleza kuwa: “Ninachowaeleza hivi sasa, kama Malkia wenu na kama bibi, nasema haya kutoka kwenye moyo wangu. Kwanza, natoa heshima kubwa kwa Diana. Alikuwa mtu wa kipekee na binadamu mwenye kipaji.”

Prince William na Kate
Prince William na Kate

Ndoa ya mjukuu wake Prince William kwa Kate Middleton ilionyesha hiba ya ujana kwa taasisi hii ya enzi na enzi.

Wakati + Prince Harry alipomuoa muigizaji wa kimarekani Meghan Markle, Elizabeth alikuwa kiongozi wa familia ambaye alionekana kwenda ambayo ilikwenda na wakati katika umaarufu, mabadiliko na ulimwengu.

Lakini kulikuwa na maumivu siku za usoni. Mtoto wake wa pili wa kiume Prince Andrew alikuwa akichunguzwa akihusisha na mashtaka yaliyomhusu mtuhumiwa wa ngono kwa watoto.

Prince Harry na Mkewe Meghan
Prince Harry na Mkewe Meghan

Harry na Meghan waliamua kujiondoa kwenye familia ya kifalme huku kukiwa na shutumba za ubaguzi.

Kifo cha mume wake Elizabeth, Prince Phillip mwaka 2021 kilimuacha na picha ya kudumu: malkia ambaye anaomboleza peke yake – wakati janga la corona lilipoingia katika taifa lake.

Mwezi Septemba alimteua waziri mkuu wa tano wa Uingereza chini ya himaya yake – ikiwa ni tukio lake la mwisho la umma.

FILE -Malkia Elizabeth (Frank Augstein/Pool via Reuters)
FILE -Malkia Elizabeth (Frank Augstein/Pool via Reuters)

Malkia Elizabeth atakumbukwa kuwa ni mkuu katika history ya moja ya mataifa makubwa sana duniani, ikiwa ni daraja kati ya mataifa ambayo yalikuwa chini ya ukoloni wa Uingereza na mustakbali wa baadaye kama wahusika wakuu katika dunia inayobadilika sana kutoka ile ambazo yeye alizaliwa na ilivyo sasa.

FILE - Malkia Elizabeth II alipotembelea Ujerumani.
FILE - Malkia Elizabeth II alipotembelea Ujerumani.


Alipoitembelea Ujerumani mwaka 2015, alizungumzia kuhusu mabadiliko makubwa aliyoshuhudia.

Malkia Elizabeth II alimwambia rais: “Katika maisha yetu Rais, tumeona mambomabaya sana na pia mazuri katika bara letu. Tumeshuhudia jinsi mambo kwa haraka yanavyoweza kubadilika kwa uzuri, lakini pia tunafahamu kwamba tufanye kazi kwa bidi ili kuendeleza mafanikio yaliyopatikana baada ya vita vya dunia.”

Familia ya Malkia wa Uingereza
Familia ya Malkia wa Uingereza

Utamaduni wa ufalme wa Uingereza – ambao Elizabeth aliushikilia – sasa uko katika mikono ya wale watakao mrithi.
Lakini Uingereza inarithi jambo moja tofauti sana katika misingi ya demografia, utamaduni na uchumi.

Katika ulimwengu, dunia hii, kazi yao ni kuonyesha sura ya ukubwa ambayo haina mikanganyiko.

XS
SM
MD
LG