Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:06

Malkia Elizabeth na familia wahudhuria ibada ya ukumbusho wa Prince Philip


Malkia Elizabeth akiwasili kwa ibada ya kumkumbuka Mumewe, Prince Philip, katika ukumbi wa Westminster Abbey.
Malkia Elizabeth akiwasili kwa ibada ya kumkumbuka Mumewe, Prince Philip, katika ukumbi wa Westminster Abbey.

Familia ya kifalme ya Uingereza Jumanne ilihudhuria ibada ya ukumbusho ya marehemu mume wa Malkia, Prince Philip, kwenye ukumbi wa Westminster Abbey karibu mwaka mmoja baada ya kifo chake.

Mazishi ya Philip yalifanyika chini ya masharti ya kukabiliana na maambukizi ya Corona na hivy kupelekea kupunguzwa kwa shughuli nyingi.

Malkia Elizabeth II ambaye anaugua, amejitokeza hadharani kwa mara ya kwanza baada ya miezi kadhaa.

Hakuwa amehudhuria hafla ya hadhara ya hali ya juu tangu alazwe hospitalini mwezi Oktoba mwaka jana.

Duke of Edinburgh, ambaye alikuwa mumewe malkia Elizabeth kwa miaka 73, alifariki tarehe 9 mwezi Aprili mwaka jana, wiki chache tu kabla ya kufikisha umri wa miaka 100. Alikuwa anaugua ugonjwa wa moyo.

XS
SM
MD
LG