Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 04:53

London yafungua michezo ya Olimpiki kwa shangwe


Watu wapatao billioni 40 kote duniani waliangalia ufunguzi wa michezo ya Olimpiki katika televisheni

Uingereza ilifungua michezo ya Olimpiki ya mwaka 2012 Ijumaa kwa mbwembwe za ndege za kivita zikipita juu ya uwanja, maonyesho ya fataki na halaiki iliyoonyesha historia ya michezo hiyo kuanzia 1896 mpaka sasa.

Karibu watazamaji 60,000 walishuhudia mwigizaji aliyevalia kama Malkia Elizabeth mwenye umri wa miaka 86 akiingia katika uwanja wa Olimpiki kwa parachuti akifuatana na mcheza sinema za James Bond - Daniel Craig. Muda mchache baadaye Malkia mwenyewe alisimama kimya wakati watoto wanaimba wimbo wa taifa "God Save the Queen"

Baadaye kidogo gwaride la mataifa lilifuatia huku wanamichezo zaidi ya 10,000 wakiingia uwanjani na kupita mbele ya jukwaa kuu. Mataifa 204 yanashiriki katika michezo ya mwaka huu.

Mashindano hayo ya siku 17 katika michezo 26 yanaanza Jumamosi na kuendelea mpaka August 17.

XS
SM
MD
LG