Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 19:17

Maelfu wajitokeza London kusherehekea miaka 70 ya utawala wa Malkia Elizabeth


Malkia wa Uingereza Elizabeth.
Malkia wa Uingereza Elizabeth.

Maelfu ya watu wa Uingereza waliwasili katikati ya mji mkuu wa London kuhudhuria sherehe za kihistoria za miaka 70, wakimshangilia Malkia Elizabeth.

Malkia alijitokeza katika shamrashamra hizo kwenye baraza la kasri ya Buckingham kutoa heshima zake katika gwaride la kijeshi akiwa amevalia nguo ya rangi ya samawati na gloves mikononi.

Waingereza wengi waliowasili katika sherehe hizo za siku nne wanachukulia sherehe hizo kama ndio mwanzo wa mwisho wa enzi ndefu ya kiongozi huyo ambaye ndiye mfalme aliyetawala kwa muda mrefu Uingereza.

Wengi wa mashabiki wa utawala wa kifalme walianza kukusanyika nje ya uwanja wa kasri ya mfalme tangu jana usiku ili kuweza kumshuhudia malkia akijitokeza na kuona gwaride ikipita katika njia muhimu za London. .

Kulikuwa na shaka ikiwa Malkia Elizabeth mwenye umri wa miaka 96 atajitokeza kwenye sherehe hizo kutokana na hali yake ya afya na matatizo ya kutembea.

Familia ya malkia ilikuwa pamoja naye kwenye baraza la kasri kutizama na kutoa heshima katika gwaride la kijeshi na maonyesho ya ndege za kijeshi.

Kwa kawaida Malkia Elizabeth angepanda farasi na kupokea heshima za kijeshi katika gwaride lakini miaka ya karibuni imekuwa tofauti na hivi leo amebaki katika jumba la kifalme.

XS
SM
MD
LG