Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 19:23

Uingereza : Prince Philip afariki dunia akiwa na umri wa miaka 99


 Prince Philip
Prince Philip

Prince Philip wa Uingereza mume wa Malkia Elizabeth II amefariki Ijumaa akiwa na umri wa miaka 99.

Prince Philip ambaye pia ni Duke wa Edinburgh ni mwanafamilia aliyehudumu kwa muda mrefu katika historia ya Uingereza na mwanafamilia ya kifalme ambaye ni mtu mzima zaidi.

Malkia Elizabeth na Malkia Elizabeth
Malkia Elizabeth na Malkia Elizabeth

Habari za kifo chake zimekuja takriban miezi miwili baada ya Prince Philip kulazwa katika hospitali ya King Edward VII mjini London hapo Februari 16.

Wakati huo ilielezewa kuwa Philip alikuwa hajisikii vizuri. Alikaa hospitali kwa siku chache kufanyiwa uchunguzi na kupumzika na baadaye alirejea nyumbani huko Windsor Castle mwezi March.

Prince Philip alizaliwa June 21, mwaka 1921. Alimuoa Malkia Elizabeth zaidi ya miaka 73 iliyopita hapo November 20 mwaka 1947.

XS
SM
MD
LG