Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 00:19

AU yatangaza kununua chanjo za Johnson & Johnson


 Mkuu wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa  Afrika Dr. John Nkengasong
Mkuu wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa  Afrika Dr. John Nkengasong

Umoja wa Afrika umeacha mipango ya kununua chanjo za COVID-19 kutoka Taasisi ya Serum ya India kwa ajili ya mataifa ya Afrika na inachunguza juu ya chanjo ya Johnson & Johnson, mkuu wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa ya Afrika alisema Alhamisi .

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters taasisi hiyo bado itasambaza chanjo ya AstraZeneca Afrika kupitia kituo cha ushirikiano wa chanjo cha COVAX, mkuu huyo wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika John Nkengasong aliwaambia waandishi wa habari, lakini Umoja wa Afrika utaagiza chanjo zaidi kutoka kwa Johnson & Johnson.

Kauli hiyo inakuja siku moja baada ya wasimamizi wa dawa Ulaya na Uingereza kusema wamegundua uhusiano kati ya chanjo ya AstraZeneca na ripoti za visa adimu vya kuganda kwa damu kwenye ubongo, lakini walisisitiza umuhimu wake katika kulinda watu.

Nkengasong alisema uhusiano huo wa watu kuugua hauhusiani na uamuzi wa Umoja wa Afrika. Kundi hilo la nchi wanachama 55 lilibadilisha juhudi zake na kuzielekeza kwenye chanjo ya Johnson & Johnson, alisema, akinukuu mpango uliotiwa saini wiki iliyopita kupata hadi dozi milioni 400 kuanzia robo ya tatu ya mwaka huu.

XS
SM
MD
LG