Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:04

Prince Philip wa Uingereza azikwa


Malkia wa Uingereza Elizabeth II akishuhudia jeneza la mumewe Prince Philip katika ibada ya mazishi iliyofanyika Kanisa la Mtakatifu George, Windsor, Uingereza April 17, 2021. Jonathan Brady/Pool via REUTERS
Malkia wa Uingereza Elizabeth II akishuhudia jeneza la mumewe Prince Philip katika ibada ya mazishi iliyofanyika Kanisa la Mtakatifu George, Windsor, Uingereza April 17, 2021. Jonathan Brady/Pool via REUTERS

Maziko ya Prince Philip mume wa Malkia Elizabeth yamefanyka Jumamosi baada ya ibada katika kanisa la St George kwenye Kasri ya Winsdor.

Maziko yamefanyika chini ya masharti makali ya kupambana na ugonjwa wa COVID-19 ambapo ni watu 30 pekee waliyo hudhuria na kufuatiliwa na mamilioni ya watazamaji kupitia televisheni.

Mapema Leo ibada ya mazishi ya Prince Philip mume wake malkia Elizabeth inafanyika Jumamosi katika kanisa la St George katika kasti ya Winsdor.

Prince Charles wa Uingereza na wanafamilia wengine wameongoza mazishi ya Prince Philip, wakati jeneza lake likisafirishwa na gari maalum la kijeshi kanisani likisindikizwa kwa miguu na familia ya kifalme.

Sherehe zote za kifalme zimekuwa zikifanyika tangu mchana wa Jumamosi kukiwa na heshma za kijeshi na mizinga 21 kupigwa, huku baadhi ya raia wakikusanyika kando ya kasri kujaribu kutoa heshima zao za mwisho.

Philip anaefahamika kama Duke of Edinburg alifariki April 9 akiwa na umri wa miaka 99.

Alimuoa Malkia Elizabeth miaka 73 iliyopita hapo mwaka 1947 na kumsaidia mke wake kubadili uongozi wa kifalme kufuatana na mabadiliko duniani baada ya vita vya pili vya dunia.

XS
SM
MD
LG