Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:22

Mfalme Charles III arejea London na mkewe Malkia Consort


Mfalme Charles III akiwa na mkewe Camilla anbaye sasa ni Malkia Consort. September 3, 2022. Reuters.
Mfalme Charles III akiwa na mkewe Camilla anbaye sasa ni Malkia Consort. September 3, 2022. Reuters.

Mfalme Charles III amerejea London leo na mkewe Camilla ambaye sasa ni Malkia Consort , kabla ya kukutana na waziri mkuu na kutoa taarifa kwenye televisheni.

Kifo cha Malkia aliyetawala kwa muda mrefu zaidi nchini Uingereza na kuwepo kama kinara katika jukwaa la dunia kwa miaka 70 kimepelekea salamu za rambirambi kutoka kote ulimwenguni.

Ni siku ya kwanza kuamka bila kuwa na mwanamke ambaye aliwahi kuelezewa na mjukuu wake wa kiume Harry kama “bibi wa taifa”, wakaazi wa uingereza walianza kukusanyika tena nje ya kasri za Buckingham na Windsor Castle kuweka maua na kupiga picha za kumbukumbu.

Mabango kote katika mji yameonyesha ujumbe wa kutoa pole na magazeti katika kurasa zake za mbele yamechapisha picha ya ujumbe wa kumkumbuka Malkia. Utawala wa Buckingham umesema kutakuwa na muda wa maombolezo na washirika wa familia na nyumba ya kifalme hadi wiki moja baada ya mazishi tarehe ambayo haijathibitishwa lakini inatarajiwa katika muda wa siku 10.

Waziri mkuu Liz Truss alisema kifo cha Malkia Elizabeth wa II kimesababisha huzuni kubwa . Truss alizungumza wakati wa kuanza kikao maalumu cha bunge cha kumuenzi malkia huyo. Alimwita Malkia mwanadiplomasia mkuu wa taifa na akasema kujitolea kwake kwa wajibu ni mfano kwa kila mtu.

XS
SM
MD
LG