Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 11:44

Uingereza yaeleza Russia imepata pigo kubwa kwa kupoteza marubani wenye uzoefu


Mahasimu wa kivita Rais Vladimir Putin (kushoto) and Volodymyr Zelenskyy
Mahasimu wa kivita Rais Vladimir Putin (kushoto) and Volodymyr Zelenskyy

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema Jumatatu kwamba hasara iliyopata Russia kupoteza marubani wenye uzoefu wakati wa uvamizi wa Ukraine imechangia kwa Russia “kupoteza nguvu za mashambulizi ya anga  kuongezewa na  mafunzo duni.”

Pia imeongeza kuwa sababu nyingine ni “kuongezeka kwa hatari za kuendesha mashambulizi ya anga kwa karibu katika eneo lenye vitu vingi katika maeneo ya ulinzi wa anga."

Uingereza imesema uwezo wa jeshi la anga la Russia “ unaweza kubadilika katika miezi michache ijayo,” katika habari mpya iliyobandikwa kwenye Twitter. “Russia kupoteza ndege zake huenda kumeiondolea uwezo mkubwa wa kutengeneza ndege mpya. Muda unaohitajika kwa mafunzo kupata marubani mahiri pia unapunguza uwezo wa Russia kufufua uwezo wake wa mashambulizi ya anga.

Huko Kherson Jumapili, wakazi walikuwa hawana umeme wala maji, wakati maafisa waliowekwa na Russia katika mji huo walikuwa wakiishutumu Ukraine kwa “kufanya hujuma,” bila ya kutoa ushahidi.

Maafisa wanaoungwa mkono na Kremlin walisema shambulizi lililoandaliwa na Ukraine, liliharibu “nguzo tatu za laini za kusambaza umeme wenye nguvu ya juu.”

Mamlaka husika zilisema wataalam wa nishati walikuwa wanashughulikia kwa “haraka” kutatua suala hilo, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

Kiza cha tanda Ukraine kutokana na uharibifu wa miundombinu ya umeme inayofanywa na Russia.
Kiza cha tanda Ukraine kutokana na uharibifu wa miundombinu ya umeme inayofanywa na Russia.

Lakini, Yaroslav Yanushevych, mkuu wa Ukraine katika uongozi wa mkoa wa Kherson, aliilaumu Russia kwa hali hiyo ya kukatika kwa umeme.

Yanushevych aliandika katika ujumbe wa Telegram: “Katika mji unaokaliwa kimabavu wa Beryslav, kuwa majeshi ya Russia yalilipua laini za umeme wa nguvu ya juu. Takriban kilomita moja na nusu ya nguzo na laini za kusambaza umeme ziliharibiwa.

“Uharibifu huo ni mkubwa,” aliongeza, kulingana na shirika la habari la AFP.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy na maafisa wengine walisema katika mwezi uliopita kuwa kati ya miundo mbinu ya umeme asilimia 30 hadi 40 ya Ukraine imeharibiwa na mashambulizi ya anga ya Russia.

Alisema katika hotuba yake ya Jumapili usiku, “Kuanzia jioni hii, shughuli za kuimarisha umeme zinaendelea huko Kyiv na mikoa mingine sita. Zaidi ya watumiaji milioni 4.5 hawana umeme. Wengi wao wako Kyiv na mkoa wa Kyiv. Kwa kweli hali ni ngumu.”

Huko Kyiv, Meya Vitali Klitschko aliwatahadharisha wakazi wa mji huo Jumapili kuwa lazima wajiandae na hali mbaya zaidi katika kipindi hiki cha baridi – kama vile kutokuwa na umeme, maji au joto katika hali ya baridi kali sana – iwapo Russia itaendelea kushambulia miundombinu ya umeme nchini humo.

“Tunafanya kila linalowezekana kuzuia hili. Lakini tuwe wakweli , maadui zetu wanafanya kila wawezalo kuhakikisha mji huu uwe hauna umeme, joto, bila maji, kwa jumla ili sote tufe. Na mustakbali wa nchi hii na mustakbali wa kila mmoja wetu unategemea ni namna gani tumejiandaa kukabiliana na hali tofauti,” Klitschko alikiambia chombo cha habari cha serikali.

Habari hii imechangiwa na taarifa za mashirika ya habari ya AP, Reuters na AFP.

XS
SM
MD
LG