Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 27, 2025 Local time: 15:48

Maseneta wawili wa Marekani wakutana na familia katika mji mkuu wa Ukraine

Seneta wa Marekani Chris Coons, kushoto, akisalimiana na mfanyakazi wa kujitolea wakati wa ziara yake katika kituo cha usambazaji cha Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani mjini Kyiv, Ukraine, Alhamisi, Novemba 3, 2022.

Maseneta wawili wa Marekani wamekutana na familia katika mji mkuu wa Ukraine na kuahidi kuendelea kutoa misaada ya kibinadamu kwa nchi hiyo iliyokumbwa na vita huku majira ya baridi kali yakikaribia.

Seneta Mdemokrat Chris Coons na Mrepublikan Rob Portman walisisitiza kujitolea kwao kwa watu wa Ukraine walipokuwa wakizungumza na familia zinazojiandaa kwa msimu wa giza, baridi na ukosefu wa joto na umeme.

Maafisa wa Ukraine wanasema mashambulizi ya Russia katika miundombinu ya nishati yameharibu asilimia 40 ya mfumo wa nishati nchini humo, na kukata nishati ya umeme kwa maelfu ya watu. Safari ya Coons na Portman siku ya Alhamisi ilikuja chini ya wiki moja kabla ya uchaguzi muhimu wa katikati ya muhula wa Marekani. Coons alisema uchaguzi huo hautaathiri uungwaji mkono wa siku zijazo kwa Ukraine, bila kujali matokeo yake.

XS
SM
MD
LG