Ripoti ilisema kuwa “Russia huenda inahangaika kutoa mafunzo ya kijeshi kwa uhamasishaji wake wa sasa na uandikishaji wa wanajeshi wakati wa kipindi hiki kila mwaka. Jeshi la Russia lilikuwa tayari limeelemewa kwa mafunzo wanayotoa kwa takriban wanajeshi 300,000 wanaohitajika kama sehemu ya uhamasishaji unaoendelea, uliotangazwa Septemba.
“Masuala haya,” wizara hiyo imesema, “yatazidi kugubikwa na uandikishaji wa ziada wa kawaida kwa kipindi hiki cha mzunguko wa kila mwaka” ambacho kinaanza Novemba kwa kusajili takriban wanajeshi 120,000.
Russia imeamua kutoa mafunzo kwa wanajeshi wake huko Belarus, wizara hiyo ilisema, “ kutokana na uhaba wa wakufunzi, silaha na vifaa nchini Russia.” Taarifa mpya za kijasusi zilisema, “kupeleka wanajeshi wenye mafunzo kidogo au bila mafunzo kunatoa uwezo mdogo wa mapambano katika vita.”
Wakati huo huo, Marekani imetoa kiasi cha dola milioni 400 kwa ajili ya msaada wa usalama kwa Ukraine wakati vita dhidi ya uvamizi wa Russia vikiingia mwezi wa tisa.
Wizara hiyo ya Ulinzi ilisema katika taarifa yake kwamba msaada wa hivi karibuni “unaonyesha umuhimu wa Marekani katika nia yake ya dhati ya kuisaidia Ukraine kukidhi mahitaji yao muhimu ya haraka sana, wakati pia ikilijengea jeshi la ulinzi la Ukraine kuwa na uwezo wa kuulinda uhuru wao kwa kipindi kirefu.”
Marekani hivi sasa imeshatoa zaidi ya dola bilioni 18.2 kwa Ukraine tangu kuanza kwa uvamizi wa kikatili usiyokuwa na sababu yoyote wa Russia hapo Februari 24,” taarifa hiyo ilieleza.