Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 11:35

Viongozi wenye hekima duniani wasisitiza mazungumzo na diplomasia kumaliza vita vya Ukraine


Zeid Raad Al Hussein, kushoto, Mary Robinson, wapili kulia, and Ernesto Zedillo, kulia, Katibu Mkuu wa zamani wa UN Ban Ki-moon akizungumza na waandishi wa habari wa shirika la habari la AP, New York, Nov. 4, 2022.
Zeid Raad Al Hussein, kushoto, Mary Robinson, wapili kulia, and Ernesto Zedillo, kulia, Katibu Mkuu wa zamani wa UN Ban Ki-moon akizungumza na waandishi wa habari wa shirika la habari la AP, New York, Nov. 4, 2022.

Mazungumzo na diplomasia  pekee ndiyo vinaweza kumaliza vita vibaya nchini Ukraine, huku ikiwa haiwezekani ushindi kamili kupatikana katika vita kwa pande zote zinazopigana, wanachama wa kikundi maarufu cha viongozi wenye hekima duniani kilichoundwa na Nelson Mandela walisema Ijumaa.

Kikundi hicho, maarufu kama Wazee, kilifikisha ujumbe huo kwa Rais Volodymyr Zelenskyy, wakimwambia wakati wa ziara yao mjini Kyiv katika kipindi hiki cha majira ya joto kwamba ni lazima aanze kufikiria njia ya kumaliza vita hivi, Rais wa zamani wa Ireland Mary Robinson ambaye anaongoza kikundi hiki maarufu The Elders alisema katika mkutano na viongozi wa shirika la habari la AP.

“Tunahitajika kushawishi fikra zaidi namna vitakavyo malizika ili kufikisha wazo la kwamba hili lazima limalizike, kinyume na kuongeza mapambano ya makombora ya kijeshi kutoka kila upande na kuangamiza watu nchini Ukraine,” alisema Robinson, ambaye alihudumu kama kamishna wa masuala ya haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa.

Viongozi hao wamelaani uvamizi wa Russia wa Februari 24 nchini Ukraine kama ni “ukiukaji mkubwa wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa na uharibifu, vitendo vya uchokozi visivyo vya haki ambavyo vinatishia kudumaza amani na usalama wa dunia.” Mwishoni mwa Septemba, Viongozi hao pia waliilaani Russia kujiingiza kimabavu katika mikoa minne ya Ukraine na kutetea haki ya Ukraine kulinda mipaka yake na uhuru wake.

Zeid Ra’ad al-Hussein, kamishna wa zamani wa haki za binadamu wa UN, alikubali kuwa diplomasia na mashauriano ndiyo njia pekee ya kumaliza vita, lakini alisisitiza kwamba hii haimaanishi kuitaka Ukraine kukubali kunyang’anywa uhuru wake, kwani Ukraine ni muathirika wa uvamizi wa Russia bila ya sababu yoyote.

Alidokeza kwamba suluhisho la kumaliza vita huenda badala yake likaihusisha Russia kupata unafuu “kutoka upande mwingine” ikielekea kuilenga NATO, au moja ya wanachama wake wakuu. Rais wa Russia Vladimir Putin kwa kipindi kirefu amekuwa akilalamika muungano wa Magharibi umekuwa ukijisogeza zaidi katika mipaka yake, ukweli ambao ameueleza katika kuhalalisha uvamizi huo.

Rais wa zamani wa Mexico Ernesto Zedillo alisema kuwa licha ya Umoja wa Ulaya na Marekani kuweka vikwazo vya uchumi “mtiririko wa rasilimali kufadhili vita hivi umeendelea,” ikiwemo mmiminiko mkubwa wa mapato ya mafuta kwa Russia.

“Nafikiri inatakiwa kupunguza unafiki katika njia ambayo vita hivi vya kishindo vya kiuchumi vinapiganwa,” alisema.

Zedillo pia aliishutumu Russia kwa vitendo vya uhalifu ambavyo Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu inajukumu la kushughulikia – mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu – na hilo ni lazima liamuliwe kwa “kufuata sheria.”

XS
SM
MD
LG