Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 23:31

Wabunge wa Ulaya watembelea Taiwan, wachukua msimamo tofauti na ule wa Chansela Scholz


Chansela Scholz na mwenyeji wake Rais Xi Jinping
Chansela Scholz na mwenyeji wake Rais Xi Jinping

Changamoto za kuunda msimamo wa pamoja kwa nchi za Ulaya katika uhusiano wake na China zilijitokeza wiki hii wakati Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz alipofanya ziara ya ngazi ya  juu Beijing.

Wakati huo huo wabunge kutoka nchi saba za Ulaya na Umoja wa Ulaya wamekuwa wakihitimisha ziara yao ya mshikamano nchini Taiwan.

Wabunge hao nane – kutoka Ubelgiji, Uingereza, Jamhuri ya Czech, Ujerumani, Kosovo, na Uholanzi, Ukraine na Bunge la Ulaya – wakiwa katika IPAC, Ushirikiano wa Mabunge Duniani juu ya hali ya China. Kikundi hicho kilianzishwa miaka miwili iliyopita kikiwa na lengo la kutoa tahadhari kwa serikali zao kwa kile wanachokiona kuwa ni tishio la China kwa amani na demokrasia kwa sababu kinaongozwa na chama cha kikomunisti cha China.

Kikundi hicho kilikutana na Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen, ambaye aliwashukuru kwa kazi yao ya kuimarisha mahusiano ya kisiasa na kiuchumi kati ya nchi zinazofuata demokrasia na Taiwan. Tsai alipewa zawadi ya shati la kitamaduni linalojulikana kama vyshyvanka lililotolewa na mbunge wa Ukraine Mykola Kniazhytskyi, wakati Waziri wa Mambo ya Nje Joseph Wu alipewa jozi ya glovu za ndondi zilizokuwa zimesainiwa na kaka Vitali na Wladimir Klitschko, mabingwa wa zamani wa ndondi ambao wamepata umaarufu zaidi kufuatia vita vya Russia na Ukraine. Vitali Klitschko pia anajulikana kama meya wa zamani wa Kyiv.

“Asanteni kwa kutufikishia moyo wa kupambana wa Ukraine hapa kwetu Taiwan. Tunashikamana na kupambana na udikteta,” Wu alisema katika taarifa aliyoiposti katika mitandao ya kijamii, pamoja na picha yake akiwa anavaa glovu hizo tayari kwa mapambano.

Els Van Hoof, mwakilishi wa bunge la Ubelgiji, alisema Alhamisi katika mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na wabunge wa IPAC huko Taipei. “Usalama wa Taiwan – na usalama wa demokrasia zetu zote – unakua kwa ushirikiano imara,” alisema. “Tutashinikiza kuongeza idadi ya ziara za bunge la pamoja kati ya Taiwan na mabunge yetu, kusaidia maelewano yetu ya pamoja na ushirikiano.”

Wabunge wa IPAC pia wako tayari “kulifanyia kazi ushirikiano munasaba wa kijeshi na ulinzi kati ya nchi zetu na Taiwan,” wakati tukishinikiza kuwepo Taiwan yenye kujihusisha zaidi na taasisi za kimataifa na kuongeza ushirikiano wa pande mbili wa kibiashara, Van Hoof alisema.

Mbunge wa Uholanzi Sjoerd Wiemer Sjoerdsma aliiambia
VOA kabla ya kuondoka Taipei Ijumaa kuwa alikuwa amevutiwa na uthabiti na matumaini aliyoshuhudia wakati wa ziara yake.

“Bila s haka, hisia ya umuhimu kati ya viongozi wao ni ya kweli,” alisema.

Viongozi wa Taiwan, alieleza, wana nia ya dhati ya kupunguza mvutano na wanatafuta ushirikiano wa kimataifa ili kuweza kufikia hili, wakati wakijiandaa kwa hali itakayajitokeza “ambapo vitisho vya kiongozi wa chama cha kikomunisti cha China siyo tu ni porojo la siasa.”

Ujumbe huo ulikuwa umeongozwa na Reinhard Buetikofer, mwanachama wa chama cha Green ambaye alikuwa miongoni mwa wabunge 10 wa Ulaya waliowekewa vikwazo na Beijing Machi 2021 kwa kile wizara ya mambo ya nje ya China ikieleza wanaleta madhara makubwa kwa uhuru wa China na maslahi yake “na kwa kebehi wanaendeza uongo na taarifa potofu.” Hatua hiyo ilifuatia vikwazo vya pamoja vilivyowekwa na EU dhidi ya China kutokana na rekodi yake Beijing ya kukiuka haki za binadamu.

Huko Taipei, serikali hiyo ilimpa Buetikofer nishani ya Grand Medal of Diplomacy kwa “azma ya kusimamia demokrasia, kuimarisha mahusiano ya Taiwan na EU na kuunga mkono ushiriki wetu wa kimataifa.”

Wakati wabunge wa IPAC wakimaliza ziara yao Taiwan, Chansela Scholz alikuwa tayari ameelekea Beijing akiwa pamoja na baadhi ya wafanyabiashara maarufu. Akikabiliwa na ukosoaji juu ya ziara hiyo nyumbani, alijitetea kufanya ziara hiyo katika makala ya maoni ya hivi karibuni iliyochapishwa kwa pamoja na magazeti ya Frankfurter Allgemeine Zeitung na Politico.

Akikiri kuhodhi kwa kuhodhi utawala wa Chama cha Kikomunisti na madaraka chini ya kiongozi wa China Xi Jinping, Scholz aliandika kuwa “imekuwa hivyo hasa kwa sababu ‘ni kazi kama kawaida’ si tena hiari kwa hali ilivyo hivyo nasafiri kwenda Beijing.”

“Matokeo ya mkutano mkuu wa chama cha kikomunisti ambao umemalizika siyo iliyojifumba: Ahadi za itikadi za Marxism-Leninism zimechukua nafasi kubwa zaidi kuliko ilivyokuwa katika mikutano iliyopita … wakati China ikibadilika, namna ya kushirikiana na China lazima ibadilike, pia,” Scholz alisema.

XS
SM
MD
LG