Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 11:07

Rais wa China XI aahidi kuendeleza sera kali ya serikali kudhibiti COVID


Rais wa China Xi Jinping akihutubia mkutano wa 20 wa chama cha Kikomunisti cha China
Rais wa China Xi Jinping akihutubia mkutano wa 20 wa chama cha Kikomunisti cha China

Rais wa China Xi Jinping ameahidi tena sera kali ya serikali ya kudhibiti COVID wakati akihutubia katika  mkutano wa 20 wa chama cha Kikomunisti cha China Jumapili.

Wachambuzi wanasema kauli hiyo inaweza kuwasikitisha watu wengi waliokuwa wakitarajia Xi ataachana na vikwazo vikali ambavyo vimewazuia wageni kuingia nchini na kuzorotesha ukuaji wa uchumi.

Sera hiyo inalaumiwa kuwa imechangia uhaba wa usambazaji wa bidhaa na kuchelewesha kufufua sekta ya usafiri wa anga na utalii.

“Licha ya kila mtu kuona kuwa uchumi umezorota, yeye bado anataka kuendeleza sera kali za kudhibiti COVID. Hii itawaumiza watu katika maisha yao,” alisema Simon Chen, mhadhiri wa sayansi ya siasa Chuo Kikuu cha Taiwan.

Tafrija ya kufunguliwa kwa mkutano wa 20 wa chama cha Kikomunisti cha China October 16, 2022.
Tafrija ya kufunguliwa kwa mkutano wa 20 wa chama cha Kikomunisti cha China October 16, 2022.

Wafuatiliaji wa mambo walitabiri kuwa hata pale maambukizi ya COVID na idadi ya vifo ilivyokuwa chini, China haijafungua mipaka yake na kurejesha hali kuwa ya kawaida kwa sababu Beijing inakataa kuruhusu kuingizwa chanjo zinazotumika zaidi zilizotengenezwa na makampuni ya nchi za Magharibi, kama vile Pfizer-BioNtech na Moderna.

China imeendelea kutegemea chanjo zinazotengenezwa ndani ya nchi na baadhi ya wafuatiliaji wa mambo wanaona Rais Xi kusisitiza kuwepo sera kali ya kudhibiti COVID ni ushahidi kuwa serikali yake haiamini kuwa chanjo zake zinaweza kuwalinda watu kutokana na wimbi jipya la maambukizi yanayotarajiwa kuanza kipindi cha baridi.

Zaidi ya miaka miwili ya janga la corona kupita , China mpaka sasa haijapitisha chanjo iliyokuwa inanguvu zaidi ya mRNA, badala yake imeamua kutumia chanjo yake inayotengeneza dhidi ya COVID-19. (AP Photo/Ng Han Guan)
Zaidi ya miaka miwili ya janga la corona kupita , China mpaka sasa haijapitisha chanjo iliyokuwa inanguvu zaidi ya mRNA, badala yake imeamua kutumia chanjo yake inayotengeneza dhidi ya COVID-19. (AP Photo/Ng Han Guan)

“Iwapo atasitisha sera hiyo kali ya kudhibiti COVID, matatizo makubwa yanaweza kutokea,” alisema Chen, akiongeza kuwa China inaweza pia kuwa inajipa muda kutengeneza chanjo yake ya mRNA, ambayo inafikiriwa kuwa ni bora zaidi.

Victor Gao, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Soochow China na makamu wa rais wa kituo cha utafiti chenye makao yake Beijing kwa ajili ya China na dunia, alisema msimamo wa serikali unakusudia kuweka kipaumbele cha kuokoa maisha na kuepusha vifo.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP

XS
SM
MD
LG