Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 13:47

Putin asema Moscow inaunga mkono sera ya China moja


Rais wa Russia Vladimir Putin akizungumza na Rais wa China Xi Jinping kando ya mkutano wa viongozi wa Jumuia ya ushirikiano wa Shanghai, mjini Samarkand, Uzbekistan, Septemba 15, 2022. Picha ya AP
Rais wa Russia Vladimir Putin akizungumza na Rais wa China Xi Jinping kando ya mkutano wa viongozi wa Jumuia ya ushirikiano wa Shanghai, mjini Samarkand, Uzbekistan, Septemba 15, 2022. Picha ya AP

Rais wa Russia Vladimir Putin amemuambia mwenzake wa China Xi Jinping hii leo Alhamisi kwamba Moscow inaunga mkono sera ya Bejing ya China moja ikipinga uchochezi unaofanywa na Marekani katika kisiwa cha Taiwan.

Ameongeza kusema kwamba Russia inathamini msimamo wa China wa kutopendelea upande wowote kuhusiana na mzozo wa Ukraine.

Xi na wa Putin wamekutana kando ya mkutano wa viongozi wa Jumuia ya ushirikaino wa Shanghai, katika mji wa kale wa njia ya hariri wa Uzbekistan wa Samarkand na kujadili juu ya hali ya vita vya Ukraine, mvutano kuhusu Taiwan na kuimarisha uhusiano kati ya nchi zao mbili.

Xi nae alimuambia Putin kwamba China iko tayari kufanya kazi na Russia kama mataifa mawili makuu ya dunia.

Katika ziara yake ya kwanza nje ya China tangu kuanza kwa janga la Covid 19, Xi aliwasili katika taifa hilo la Asia ya kati Jumatano, mwezi mmoja kabla ya chama cha kikomunisti kikitarajiwa kumuinua Xi kama kiongozi wa China mwenye nguvu tangu enzi ya Mao Zedong.

Mara ya mwisho Xi na Putin kukutana ana kwa ana, ilikuwa wiki chache kabla ya Russia kuivamia Ukraine tarehe 24 Februari.

XS
SM
MD
LG