Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 00:09

Taiwan yaondoa kanuni za Covid-19 kwa watalii


Kituo cha kupimia Covid-19 mjini Taipei, Taiwan, kwenye picha ya maktaba
Kituo cha kupimia Covid-19 mjini Taipei, Taiwan, kwenye picha ya maktaba

Taiwan Alhamisi imeondoa vikwazo vyote vya covid-19 na kwa hivyo kuruhusu watalii kutembelea kisiwa hicho bila ukaguzi wowote baada ya zaidi ya muda wa miaka miwili na nusu.

Wageni waliyotembelea Hong Kong, Taiwan pamoja na China bara hapo awali, walihitajika kujiweka karantini mara baada ya kuwasili, tangu janga la corona lilipoingia, licha ya kwamba mataifa mengi yalikuwa tayari yamefungua mipaka yake kwa watalii katika miezi ya karibuni.

Sasa wageni hawatahitajika kujiweka karantini, wala kufanya vipimo, ingawa watahitajika kuangalia afya zao kwa wiki moja baada ya kuwasili. Hata hivyo watahitajika kuonyesha kutokuwa na maambukizi baada ya vipimo vya haraka, wakati wa kuwasili.

Darzeni ya watalii kutoka Thailand walikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Taiwan wa Taoyuan, mjini Taipei, saa chache baada ya tangazo hilo kutolewa.

XS
SM
MD
LG