Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 20:44

Xi asifu mafanikio ya China, atoa wito wa umoja mbele ya Kongamano kuu ya chama


Rais Xi Jingping ahudhuria sherehe za ufunguzi wa Kongamano kuu la Chama cha Kikomunisti cha China
Rais Xi Jingping ahudhuria sherehe za ufunguzi wa Kongamano kuu la Chama cha Kikomunisti cha China

Rais Xi Jingping amesifu mafanikio ya China kufikia taifa kuu duniani na kuomba kuwepo na umoja katika uwongozi wake, alipokua anafungua Kongamano Kuu la Chama cha Kikomunisti cha China Jumapili.

Akihutubia Kongamano hilo ambalo ni la kuidhinisha tu, maazimio ya Kamati Kuu ya chama katika Ukumbi Mkuu wa Wananchi, Xi, alisifu na kutetea baadhi ya sera muhimu za serikali yake ikiwa ni pamoja na kupambana na COVID, na juhudi zake za kupambana na rushwa ambazo zimewaondosha wapinzani ndani ya chama.

"Umoja ni nguvu na ushindi unahitaji umoja" alisema Xi baada ya kufika kwenye jukwa akishangiriwa na wajumbe 2 300 waloteuliwa kuhudhuria kongamano hilo, na kutarajiwa kupiga kura kuchagua wakuu wa chama kwa miaka mitano ijayo.

XI ambae ambae miaka 10 ya utawala wake imegeuza nchi na kua taifa kuu la pili duniani amesema kwamba "ushawishi wa China kimataifa, pamoja na nguvu zake na mchango wake wa kugeuza mambo duniani zimeongezeka sana."

Rais Xi Jingping wa China akihutubia ufunguzi wa mkutano mkuu wa Chama cha Kikomunist mjini Bejing.
Rais Xi Jingping wa China akihutubia ufunguzi wa mkutano mkuu wa Chama cha Kikomunist mjini Bejing.

Katika hotuba yake ya dakika 100 juu ya "ripoti ya kazi" kuhusu miaka mitano ya utawala wake, Xi alizingatia juu ya masuala mawili nyeti - usalama na uhuru wa mipaka ya nchi - hususa kuhusu Hong Kong, baada ya kukandamizwa maandamano ya kutetea demokrasia na kisiwa cha Taiwani chenye utawala wake ndani.

Alishangiliwa kwa makofi makubwa alipopongeza kipindi cha mpito cha Hong Kong kutoka "ghasia kuelekea utawala wa kisheria", huku akiahidi "kutoacha kamwe utumiaji nguvu" dhidi ya kisiwa cha Taiwan.

Kiongozi huyo anaetazamiwa kuteuliwa na wajumbe kwa mhula wa tatu - kitendo ambacho hakijawahi kufanyika chini ya China ya leo - amesifia juhudi mbali mbali za sera za utawala wake kuanzia vita dhidi ya janga la COVID, kupamnbana na ulaji rushwa ambapo maelfu ya maafisa wa chama wamehukumia vifugo vya jela, hadi kukandamiza sauti ya upinzani.

Hakutangaza sera mpya bali kuzingatia juu ya kazi alizofanya kuleta manedeleo makuba nchini mwake.

XS
SM
MD
LG