Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:22

Putin asifia ushirikiano na China, ashutumu "ubabe wa Marekani"


Rais wa Russia Vladmir Putin
Rais wa Russia Vladmir Putin

Rais wa Russia Vladimir Putin, alisema Alhamisi kwamba anaelewa kuwa China ina "maswali na wasiwasi" kuhusu vita vya Moscow nchini Ukraine, na kusifia uhusiano kati ya nchi yake na China.

Putin alisema hayo alipofanya mazungumzo na kiongozi wa China Xi Jinping nchini Uzbekistan.

Hadharani, China imechukua msimamo wa kutoegemea upande wowote kuhusiana na uvamizi wa Russia, ambao umeendelea kwa miezi 7, hata ingawa Rais Xi alisema kwamba moja ya kanuni kuu za sera ya nje ya Beijing, ni kwamba nchi zinapaswa kuheshimu mipaka ya mataifa mengine.

Katika kauli iliyopeperushwa kupitia televisheni mwanzoni mwa mazungumzo yao huko Samarkand, Putin aliiambia Xi, "Tunathamini sana msimamo wa usawa wa marafiki zetu wa China, kuhusu mzozo wa Ukraine.

Tunaelewa maswali na wasiwasi wako juu ya suala hili, na wakati wa mkutano wa leo, bila shaka tutafafanua haya yote kwa undani."

Matamshi ya Putin yalikuja wakati Ukraine, katika siku za hivi karibuni, imefanikiwa kutwaa tena maeneo makubwa, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, ambayo Russia ilikuwa imeteka katika wiki za mwanzo za vita.

Putin aliishutumu Marekani kwa msimamo wake kuhudu Taiwan na kukemea kile alichokiita ubabe wa Marekani na "azma ya kuuatawala ulimwengu" na kusema kwamba anaona Russia na China,zikishirikiana dhidi yake.

XS
SM
MD
LG