Samia amekuwa rais wa kwanza kutoka Afrika kukutana na Xi Jinping, tangu alipoidhinishwa kuongoza China kwa muhula mwingine.
Kati ya mikataba hiyo ni ujenzi wa miundo mbinu ya usafiri hasa barabara, reli na bandari.
China imetoa msaada wa shilingi bilioni 31 na nusu kwa ajili ya maendeleo ya uchumi huku Zanzibar ikipewa mkopo wa shilingi milioni 56.7 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege.
Nchi hiyo ya Afrika Mashariki vile vile ilisitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani karibu na Dar es Salaam wakati wa utawala wa hayati John Magufuli aliyesema kwamba mkataba uliokuwa umesainiwa kati ya China na Tanzania ulikuwa mbaya. Haijulikani kama ujenzi wa bandari hiyo umejadiliwa katika mkutano wa rais Samia na Xi Jinping.
Shirika la habari la China CGTN limeripoti kwamba wawekezaji wa China wana hamu kubwa ya kuwekeza katika teknolojia na viwanda karibu na bandari ya Bagamoyo na kwamba ziara ya rais Samia inatoa fursa ya kufanyika mazungumzo ya uwezekano wa China kushirikiana na Tanzania kujenga bandari hiyo na miradi mingine ya maendeleo.