Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 11:01

China imepitisha sheria kuwalinda wanawake dhidi ya manyanyaso ya ngono


Wanawake wanamichezo China wakifurahia michezo
Wanawake wanamichezo China wakifurahia michezo

Sheria hiyo inakuja wakati wanaharakati wameelezea wasiwasi wao juu ya kuongezeka kwa matamshi ya serikali juu ya thamani ya majukumu ya kiasili ya wanawake, na kile ambacho baadhi wanakiona kama vikwazo kwa haki za wanawake na mitazamo mikali kuhusu  utoaji mimba

China ilipitisha sheria siku ya Jumapili inayolenga kuwapa wanawake ulinzi zaidi dhidi ya ubaguzi wa kijinsia na manyanyaso ya ngono, siku chache baada ya mswaada kuwasilishwa katika bunge la juu nchi humo kufuatia marekebisho ya tatu na mchango mkubwa wa umma.

Sheria hiyo inakuja wakati wanaharakati wameelezea wasiwasi wao juu ya kuongezeka kwa matamshi ya serikali juu ya thamani ya majukumu ya kiasili ya wanawake, na kile ambacho baadhi wanakiona kama vikwazo kwa haki za wanawake na mitazamo mikali kuhusu utoaji mimba.

Bado haijafahamika ni kwa kiwango gani mitazamo hiyo ya ki-Conservative itaonekana katika sheria mpya. Hakuna maelezo yaliyopatika juu ya sheria hiyo zaidi ya kupitishwa kwake.

Hii ni mara ya kwanza katika kipindi cha takriban miaka 30 ambapo sheria kuhusu ulinzi wa wanawake ilibadilishwa. Ikipewa jina la "Sheria ya Ulinzi wa Haki za Wanawake na Maslahi", mswaada huo uliwasilishwa kwa Kamati ya Bunge la Wananchi (NPC) siku ya Alhamisi. NPC kwenye tovuti yake ilitangaza kwamba sheria hiyo imepitishwa.

XS
SM
MD
LG