Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 23:04

Marekani yaikosoa China na Russia kwa 'kuikingia kifua' Korea Kaskazini


Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa China Xi Jinping
Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa China Xi Jinping

Marekani imeikosoa China na Russia katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa  Ijumaa kwa “kuikingia kifua” Korea Kaskazini baada ya Pyongyang kufanya majaribio kadhaa ya makombora.

Korea Kaskazini “imekuwa ikinufaika kukingiwa kifua na wanachama wawili wa Baraza hili,” balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Linda Thomas-Greenfield, alikiambia kikao cha dharura cha baraza hilo Ijumaa, bila ya kutaja majina ya nchi hizo moja kwa moja.

FILE - Balozi wa Marekani Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield
FILE - Balozi wa Marekani Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield

“Wanachama hawa wameamua kuangalia upande mwingine ili kuhalalisha ukiukaji wa mara kwa mara wa DPRK na hivyo, wameiwezesha DPRK na kulidhihaki baraza hili,” Thomas-Greenfield alisema, akitumia jina rasmi la Korea Kaskazini, ambalo ni Democratic People’s Republic of Korea.

Korea Kaskazini imefyatua makombora 30 tangu siku ya Jumatano, ikiwemo yale yaliyosababisha tahadhari ya shambulizi la angani na kujificha katika maeneo ya dharura huko Korea Kusini na Japan. Mfululizo wa makombora hayo lilikuwa ni jaribio la Alhamisi la makombora ya balistiki yenye kusafiri kuvuka mabara, ambayo yaliripotiwa kutoweza kukamilisha safari yake.

Ufyatuaji wa makombora hayo ni majibu kwa mazoezi ya kijeshi yanayofanywa na Korea Kusini na Marekani, ambayo yamepanuliwa kufuatia jaribio la hivi karibuni la Korea Kaskazini la majaribio ya silaha na vitisho vingine.

Ndege za kivita za Korea Kusini zilizokuwa zikiruka maeneo mbalimbali baada ya kugundua ndege za kijeshi 180 za Korea Kaskazini zilikiwa karibu na mpaka huku mivutano kwenye Rasi ya Korea ikiendelea kupamba moto.

Korea Kaskazini ikijaribisha makombora yake ya nyuklia.
Korea Kaskazini ikijaribisha makombora yake ya nyuklia.

Kimnya cha Baraza kinaelezwa "kinakasirisha"

Baraza la Usalama la UN lilikutana kujadili mgogoro huo Ijumaa baada ya Marekani, Uingereza, Albania, Ufaransa, Ireland na Norway kupendekeza mkutano huo kufanyika.

Wanachama 10 ambao siyo wanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama, zikiwemo India, Brazil na Mexico, zililaani ufyatuaji wa makombora yaliyofanywa na Korea Kaskazini katika taarifa ya pamoja.

Thomas-Greenfield alieleza kuwa urushaji wa makombora ya balistiki 59 ya Korea Kaskazini mwaka huu ulikuwa “unakasirisha.”

Kikao cha Baraza la Usalama la UN
Kikao cha Baraza la Usalama la UN

“Hivyo hivyo inaudhi kuona baraza hilo likinyamazia suala hili,” alisema kuhusu nchi 15 zilizoko katika Baraza la Usalama, ambazo hazikutoa tamko au kupitisha vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini kwa vitendo vyake visivyokubalika.

Hilo linatokea kutokana na China na Russia kupinga hatua kuchukuliwa. China imekwenda mbali zaidi kutaka vikwazo dhidi ya Pyongyang vilegezwe.

Nchi zote mbili zimeeleza kuwa mazoezi ya pamoja kati ya Marekani na Korea Kusini ndiyo sababu ya kuongezeka mivutano katika Rasi ya Korea, Thomas-Greenfield alisema.

Balozi wa China ameitaka Washington Ijumaa kusitisha “yenyewe peke yake kuendesha mivutano na uchokozi” na kuonyesha ukweli wake kwa kujibu “wasiwasi halali na wa kuridhisha” wa Korea Kaskazini.

“Kwa suala la Rasi ya Korea, Baraza la Usalama linatakiwa kuchukua hatua ya kujenga badala ya siku zote kushinikiza vitisho,” Balozi Zhang Jun aliongeza.

Russia pia imeituhumu Marekani kwa kuchochea mvutano huo.

XS
SM
MD
LG