Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 10:57

Maelfu waandamana kuunga mkono chama tawala Korea Kaskazini


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un (KCNA via REUTERS).
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un (KCNA via REUTERS).

Maelfu ya watu walikusanyika katika uwanja wa Kim II Sung, mjini Pyongyang Jumatano katika uungwaji mkono kwa chama tawala cha Korea Kaskazini Workers Party na kiongozi Kim Jong Un.

Vyombo vya Habari vimeripoti leo siku moja baada ya tukio ambalo ni la kawaida Korea Kaskazini.

Vyombo vya Habari vya kigeni havikuruhusiwa kuandika juu ya tukio hilo.

Taarifa rasmi haikusema kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kama alihudhuria.

Badala yake imesisitiza kwamba Waziri Mkuu Kim Tok Hun aliongoza tukio hilo.

Mkusanyiko huo unafuatia mkutano mkubwa uliofanyika mwishoni mwa mwezi desemba .

XS
SM
MD
LG