Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 16:12

Korea Kaskazini yaipa masharti Korea Kusini kwa mazungumzo kuendelea


Kim Jong Un (Photo by STR/KCNA via KNS/AFP)
Kim Jong Un (Photo by STR/KCNA via KNS/AFP)

Dada ya Kim Jong Un, Kiongozi wa Korea Kaskazini, ambaye ana ushawishi mkubwa katika utawala wa nchi hiyo amesema Ijumaa wako tayari kurudi kwenye meza ya mazungumzo na Korea Kusini.

Lakini ametoa sharti watashiriki tu mazungumzo hayo, ikiwa Korea Kusini haitaichokoza nchi yake kupitia sera za uhasama.

Kim Yo Jong ametoa taarifa hiyo kama jibu kuelekea miito ya Rais Moon Jae In wa Korea Kusini ya kutaka azimio la kumalizika vita vya mwaka 1950 hadi 1953 kati ya Korea hizo mbili, kuwa kama njia ya kudumisha amani.

Mgogoro huo, ambao uligawanya rași hiyo kuwa nchi mbili, ulimalizika mnamo 1953 lakini mkataba wa amani uliosainiwa, umekuwa ukiyumbayumba.

Nchi hizo mbili zimekuwa kwenye vita tangu wakati huo, na mara kwa mara, zimekuwa na uhusiano wenye taharuki na malumbano. Pendekezo hilo limejiri siku chache baada ya Korea Kaskazini kufanya majaribio yake ya kwanza ya kufyatua makombora baada ya kipindi cha utulivu cha miezi sita.

"Kinachohitaji kutupiliwa mbali ni mitazamo ya kinafiki , ubaguzi, tabia mbaya na msimamo wa uhasama wa kuhalalisha matendo yao wenyewe huku wakikosoa utekelezaji wetu wa haki ya kujilinda," alisema katika taarifa.

"Ni wakati tu sharti kama hilo litakapotimizwa, itawezekana kukaa uso kwa uso na kutangaza kukomesha vita."

XS
SM
MD
LG