Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:40

Wananchi waingiwa na wasiwasi kumuona Kim Jong Un amekonda


Kim Jong Un
Kim Jong Un

Televisheni ya serikali ya Korea Kaskazini imethibitisha kupungua kwa uzito wa Kim Jong Un, na hata kukubali kuwa hali ya kiafya ya kiongozi huyo inaendelea kuwa ni suala linaloleta wasiwasi kwa Pyongyang. 


Uthibitishaji huo ulitangazwa wakati wa mahojiano na wakazi wa Korea Kaskazini yaliyofanywa na televisheni kuu ya serikali ya Korea Kaskazini, kulingana na shirika la habari la Korea Kusini Yonhap.

“Watu walikuwa wanasimanzi kumuona Katibu Mkuu huyo anayeheshimika akiwa amepungua uzito,” mkazi mmoja amesema katika mahojiano yaliyopeperushwa Ijumaa. “Kila mtu anasema anahuzuni ya kutokwa na machozi.”

Maoni hayo yalijumuishwa pasipo kufungamana na ripoti ya KCTV inayoonyesha mahojiano ya mitaani na wananchi wakieleza maoni yao juu ya masuala mbalimbali, ikiwemo maonyesho ya kitamaduni ya hivi karibuni.

Repoti hiyo haikutaja wala kuzungumzia matatizo ya afya yanayomkabili Kim. Wachambuzi wanasema, hata hivyo, uthibitisho huo wa Pyongyang kwamba hali ya kiongozi huyo imebadilika inaonekana bado ni muhimu.
.
Hali ya kiafya ya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 37 imekuwa mara kwa mara ikidadisiwa na dhana nzito, hivi karibuni baada ya kujitokeza katika televisheni ya serikali akionekana amepungua uzito zaidi kuliko vile alivyokuwa wiki kadhaa siku za nyuma.

Uvumi juu ya hali ya afya ya Kim uliongezeka mwaka 2020 baada ya kutoonekana hadharani katika sherehe za kuzaliwa zinazoadhimishwa kwa ajili ya babu yake, kiongozi muasisi wa taifa la Korea Kaskazini Kim Il Sung.

Chanzo cha Habari : VOA News

XS
SM
MD
LG