Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 21:50

Baraza la Usalama la UN laombwa kujadili Korea Kaskazini


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un

Baadhi ya wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa ikwemo Japan, wamewaomba wenzao miongoni mwa wanachama 15 kwenye baraza hilo kufanya kikao cha faragha ili kuzungumzia hali inayoendelea ya ukiukaji wa haki za binadamu Korea kaskazini.  

Balozi wa Marekani kwenye baraza hilo Linda Thomas Greenfield wakati akizungumza kwa niaba ya Marekani,Uingereza, Estonia, Ufaransa, Ireland, Japan na Norway ambao wote ni wanachama isipokuwa Japan,amesema kwamba ni lazima mwenendo wa Korea kaskazini wa kukiuka haki za binadamu pamoja na matumizi ya silaha nzito upewe kipaumbele na kukomeshwa kwa kuwa unahatarisha usalama wa kimataifa.

Mwaka 2014, ripoti kutoka kwa tume maalum ya uchunguzi iliyobuniwa na baraza hilo ilifichua hali halisi ya ukatili mkubwa dhidi ya binadamu, unaoendelea kutekelezwa Korea kaskazini. Tangu wakati huo , baraza hilo limekuwa likizungumzia hali hiyo kila Decemba licha ya baadhi ya wanachama kusema wamba halifai kushikilia jukumu hilo.

XS
SM
MD
LG