Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:02

Mkutano wa Trump, Kim wamalizika bila ya kufikia makubaliano


Rais Donald Trump, kushoto, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo,
Rais Donald Trump, kushoto, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo,

Meza ilikuwa imeandaliwa kwa ajili ya chakula cha mchana katika maandalizi ya sherehe ya tukio la kihistoria la kusaini mikataba kati ya Rais Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, katika hoteli ya Metropole, nchini Vietnam.

Lakini shughuli zote mbili hizo zilifutwa kwa haraka kabisa kabla ya kipindi cha mchana kuingia, siku ya Alhamisi, na kufanya mkutano huo wa pili wa viongozi hao wa nchi mbili kumalizika kabla ya wakati wake.

“Siku zote lazima uwe tayari kutoka nje ya mkutano,” alisema Trump, akiongeza kuwa “Ningeweza kusaini kitu fulani leo” na kuthibitisha, “tulikuwa na makaratasi yaliyokuwa yako tayari kwa ajili ya kusainiwa.”

Rais aliongeza kuwa Kim alitaka vikwazo viondolewe kwa ujumla wake na hatukuweza kufanya hivyo,” Trump alieleza katika mkutano na waandishi wa habari huko Hanoi, baada ya mazungumzo hayo kuvunjika.

“Walikuwa tayari kutokomeza silaha za nyuklia kwa kiwango kikubwa katika maeneo tuliyokuwa tunataka hilo lifanyike, lakini hatukuweza kuondoa vikwazo vyote kwa hilo.” Amesema walizungumzia kutokomeza kituo cha nyuklia cha Yougbyon, lakini jambo lenye ugumu ni eneo jingine la kinu cha kuboresha uranium.

Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo, akisimama na Trump, katika ukumbi mkubwa wa hoteli ya JW Marriott ambao ulikuwa umepambwa na mabango yaliyokuwa yanautangaza mkutano huo, amesema anatumaini kuwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili yafanyika tena muda sio mrefu.

Kulikuwa na “suala la muda na mpangilio wa masuala kadhaa” ambayo yalizuia viongozi hao wawili kuweza kumaliza mazungumzo hayo, amesema Pompeo, ambaye yeye pamoja na mshauri wa usalama wa taifa John Bolton wanaonekana ni wenye misimamo mikali katika uongozi wa Trump katika kukabiliana na Pyongyang.

XS
SM
MD
LG