Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:12

Hotuba ya Hali ya Taifa :Trump atoa wito wa mwisho juu ya ujenzi wa ukuta


Rais Trump akitoa hotuba yake katika Bunge la Marekani - Congress
Rais Trump akitoa hotuba yake katika Bunge la Marekani - Congress

Rais Donald Trump ametumia hotuba yake juu ya hali ya Taifa Jumanne usiku kuweka shinikizo la mwisho kujengwa ukuta katika mpaka wa kusini ya Marekani, wakati siku chache zilizopita alitahadharisha kuwa serikali inaweza kufungwa tena.

“Nitajenga ukuta,” Trump aliahidi, akisema ukuta wa chuma utakuwa wa kimkakati, wakisasa na wenye matundu ya kuonyesha upande wa pili. Lakini alisita kutangaza hali ya dharura ya kitaifa kwa ajili ya kupatiwa fedha za ujenzi huo.

Trump ambaye alikuwa amefanya ukuta wa mpakani ni moja ya ahadi za kampeni yake, alitumia muda mwingi wa hotuba yake kueleza hatari za mpaka wa Marekani na Mexico.

Hivi tunavyoongea, misafara mikubwa iliyoandaliwa inaelekea Marekani,” Trump amesema, akikusudia ni kikundi cha wahamiaji wanaume, wanawake na watoto kama kama uvamizi hatari.”

Katika hotuba yake Rais Trump ameeleza sera ya nje ya Marekani akigusia mikataba mbalimbali.

Sera ya biashara

Trump amesema : "Mkataba wetu mpya kati ya Marekani - Mexico -Canada -- au USMCA -- utachukuwa nafasi ya NAFTA na kuleta tija kwa wafanyakazi wa Marekani : ukirudisha ajira zetu za kazi za viwandani, ukipanuwa wigo la kilimo, na kulinda haki miliki ya uvumbuzi, na kuhakikisha kuwa magari zaidi yanaweka alama ya maneno manne ya kupendeza : Made in the USA.

Sera ya silaha za maangamizi

"Wakati tukiwa tunatekeleza makataba huo herufi kwa herufi, Russia imekuwa ikikiuka makubaliano. Ndio maana nimetangaza kuwa Marekani itajiondoa rasmi kutoka katika Mkataba wa silaha za nyuklia za masafa ya kati au INF

"Tunaweza kuanzisha mazungumzo juu ya mkataba mwengine, na kuiongeza China na nchi nyingine, au pengine hatutaweza -- kwa hali hiyo, tutaweza kuwashinda wengine wote."

"Bado kuna kazi nyingi zinatakiwa kufanyika, lakini mahusiano yangu na Kim Jong Un ni mtu mzuri. Na Mwenyekiti Kim na mimi tutakutana tena Februari 27 na 28 huko Vietnam."

Demokrasia Venezuela

Rais Trump amesema : "Wiki mbili zilizopita, Marekani imetangaza rasmi kuitambua serikali halali ya Venezuela, na Rais wa mpito Juan Guaido."

Hali ya maridhiano Afghanistan

Rais amesema kuwa : "Majeshi yetu shupavu hivi sasa yamekuwa yakipigana huko Mashariki ya Kati kwa takriban miaka 19. Huko Afghanistan na Iraq, takriban mashujaa wa jeshi letu 7,000 wamejitolea maisha yao. Zaidi ya Wamarekani 52,000 wamejeruhiwa katika vita hivyo. Tumetumia zaidi ya dola trilioni 7 huko Mashariki ya Kati.

"Hivi sasa tukiwa tunashirikiana na washirika wetu kuangamiza kikundi cha ISIS, ni wakati kuwapa mapokezi makubwa mashujaa wapiganaji wetu wanaorejea nyumbani.

"Kadhalika nimekuwa nikiharakisha mazungumzo ili kufikia maridhiano ya kisiasa huko Afghanistan. Majeshi yetu yamekuwa yakipigana kwa juhudi kubwa -- na tunawapongeza kwa ushujaa wao, hivi sasa tunaweza kuanza kutafuta suluhu ya kisiasa katika mgogoro huu wa muda mrefu uliouwa wengi."

"Kuhakikisha kuwa ufisadi wa kidikteta hautaweza kupata silaha za nyuklia, nimeiondoa Marekani kutoka katika makubaliano ya balaa kubwa ya nyuklia. Na kabla ya kuanza kipindi cha baridi tuliweka vikwazo dhidi ya Iran ambavyo havijawahi kuwekwa kwa nchi yoyote."

Trump ahimiza umoja

Trump ametoa hotuba yake katika hali ya mabadiliko : kwa mara ya kwanza spika wa Baraza la Wawakilishi kutoka chama cha waliowengi Wademokrat, Nancy Pelosi wa California, alikuwa akimtupia macho Trump nyuma ya mabega yake wakati akilihutubia Bunge la Marekani –Congress.

Wademokrat walianza kulidhibiti Baraza la Wawakilishi wakati wa uchaguzi wa katikati ya muhula Novemba ambapo kulitokea mgawanyiko katika serikali ikiwa Wademokrat ni waliowengi kaitka Baraza hilo na Warepublikan wao ni waliowengi katika Baraza la Seneti na White House kitu ambacho kimemuwiya vigumu Trump kutekeleza mapendekezo ya sera zake.

Ikiwa ni sehemu ya kutambua kwake Trump hali mpya ya kisiasa inayoendelea Marekani, Trump katika hotuba yake alijikita kuhimiza umoja na ushirikiano kati ya Warepublikan na Wademokrat. Moja ya maelezo yake, Trump alisisitiza kuwa watunga sheria lazima “ warejeshi mshikamano wa kupendana” Washington.

“Nawataka wanaume na wanawake katika Bunge hili : Angalieni fursa zilizoko mbele yetu! Mafanikio yetu yakusisimua yako mbele yetu. Safari zetu zenye mafanikio zinatusubiri.”

XS
SM
MD
LG