Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:09

Hotuba ya Trump Jumamosi : Itazungumzia kufungwa serikali, usalama wa mpakani


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump amesema atatoa tamko muhimu juu ya kufungwa kwa serikali na usalama wa mpakani wakati akilihutubia taifa Jumamosi.

Trump amesema hotuba hiyo kutoka White House ataitoa saa tisa ya mchana saa za upande wa mashariki wa Marekani na atahutubia juu ya “mgogoro wa kibinadamu ulioko upande wa mpaka wa kusini wa Marekani.”

Mvutano ulioko kati ya Wademokrat na Warepublikan juu ya kumpatia Trump fedha za kujenga ukuta katika mpaka wa Marekani na Mexico umepelekea serikali kufungwa, na imefikia siku ya 29 leo Jumamosi.

Trump anataka apatiwe zaidi ya dola za Marekani bilioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa ukuta huo, wakati Wademokrat wamempatia zaidi ya dola bilioni 1 katika malipo mapya ya kuimarisha usalama mpakani, na sio kwa ajili hasa ya ujenzi wa ukuta.

Vyanzo vya kambi ya Wademokrat vinaeleza kuwa fedha zitaingizwa katika kifungu cha muswada wa matumizi ambao utajadiliwa wiki ijayo : Dola milioni 524 kwa ajili ya kuboresha maeneo ya mipaka ambako wahamiaji wanapita na dola milioni 563 kwa ajili ya kuajiri majaji zaidi wa uhamiaji.

XS
SM
MD
LG