Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:16

Rais Trump ametetea hoja yake ya kutaka kujenga ukuta mpakani


Rais Donald Trump akilihutubia taifa. Januari 8, 2019
Rais Donald Trump akilihutubia taifa. Januari 8, 2019

Trump alisema wanawake na watoto ni waathirika wakubwa wa mfumo ulioharibika kukabiliana na usafirishaji haramu wa watu akisema idara za doria mpakani hazina tena nyumba za kuwapatia hifadhi wahamiaji na haziwezi kuendelea na utaratibu kwa watu wanaotafuta hifadhi

Rais Donald Trump anasema kuna mzozo wa kibinadamu na usalama unaoendelea kuwa mkubwa kwenye mpaka wa Marekani na Mexico akiueleza kuwa ni mzozo wa moyo na kiroho.

Katika hotuba yake ya kwanza ya kitaifa kutoka chumba cha Oval Office ndani ya White House Rais Trump alifafanua hoja yake ya kujenga ukuta kwenye mpaka wa Marekani na Mexico lakini hakutangaza hali ya dharura ya kitaifa ambayo itamruhusu kujenga ukuta bila idhini ya bunge.

VOA ilizungumza na Profesa Patrick Nighula na kutaka kujua iwapo hotuba ya Rais Trump imebeba uzito wa hoja kwa bunge na taifa anapodai apatiwe fedha za ujenzi wa ukuta hali iliyosababisha serikali kuu kufungwa hadi wakati huu.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:52 0:00

Alisema wakati wamarekani wanaumizwa kutokana na kile alichokieleza kutodhibitiwa wahamiaji haramu Rais Trump alisema wamarekani wenye asili ya Kiafrika na asili ya Amerika Kusini wanaathirika zaidi kwa sababu fursa za ajira zimechukuliwa na wahamiaji.

Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Trump alisema wanawake na watoto ni waathirika wakubwa wa mfumo ulioharibika kukabiliana na usafirishaji haramu wa watu akisema idara za doria mpakani hazina tena nyumba za kuwapatia hifadhi wahamiaji na haziwezi kuendelea na utaratibu wote kwa watu wanaotafuta hifadhi.

Baada ya maelezo hayo yote alirudia msimamo wake wa kutaka ukuta akisema hajali ikiwa ni wa senyeng’e au chuma akilitaka bunge kuidhinisha dola bilioni 5.7 ili kujenga ukota huo.

Aliwalaumu wademocrat kwa kukataa kutambua kuna matatizo kwenye mpaka na kwa mara nyingine kuwalaumu kwa kusababisha baadhi ya shughuli za serikali kuu kufungwa.

Viongozi wa chama cha democrats bungeni mara moja wakamjibu wakimlaumu kwa kuchagua kitisho kuliko suluhisho la pande zote.

Nancy Pelosi
Nancy Pelosi

Spika wa baraza la wawakilishi Nancy Pelosi amesema wademocrats wanakubaliana na haja ya kuimarisha usalama wa mpakani lakini amemlaumu Trump kwa ukaidi wake wa kutaka ukuta kabla ya kufungua serikali.

Wademocrats wanasema ni lazima shughuli za serikali kuu zifunguliwe kwanza na suala la usalama wa mpakani na ukuta lijadiliwe katika utaratibu tofauti.

XS
SM
MD
LG