Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 19:29

Hotuba ya Trump : Maeneo muhimu ya sera ya mambo ya nje ya Marekani


Hotuba ya Trump : Maeneo muhimu ya sera ya mambo ya nje ya Marekani
please wait

No media source currently available

0:00 0:04:43 0:00

Rais Donald Trump : "Hivi sasa tunaweka wazi kwa China kuwa baada ya miaka kadhaa ya kulenga viwanda vyetu, na kuiba haki miliki ya ubunifu wetu, wizi wa ajira za Wamarekani na utajiri wao umefikia ukingoni."

"Mkataba wetu mpya kati ya Marekani - Mexico -Canada -- au USMCA -- utachukuwa nafasi ya NAFTA na kuleta tija kwa wafanyakazi wa Marekani : ukirudisha ajira zetu za kazi za viwandani, ukipanuwa wigo la kilimo, na kulinda haki miliki ya uvumbuzi, na kuhakikisha kuwa magari zaidi yanaweka alama ya maneno manne ya kupendeza : Made in the USA.

"Wakati tukiwa tunatekeleza makataba huo herufi kwa herufi, Russia imekuwa ikikiuka makubaliano. Ndio maana nimetangaza kuwa Marekani itajiondoa rasmi kutoka katika Mkataba wa silaha za nyuklia za masafa ya kati au INF

"Tunaweza kuanzisha mazungumzo juu ya mkataba mwengine, na kuiongeza China na nchi nyingine, au pengine hatutaweza -- kwa hali hiyo, tutaweza kuwashinda wengine wote."

"Bado kuna kazi nyingi zinatakiwa kufanyika, lakini mahusiano yangu na Kim Jong Un ni mtu mzuri. Na Mwenyekiti Kim na mimi tutakutana tena Februari 27 na 28 huko Vietnam."

"Wiki mbili zilizopita, Marekani imetangaza rasmi kuitambua serikali halali ya Venezuela, na Rais wa mpito Juan Guaido."

"Majeshi yetu shupavu hivi sasa yamekuwa yakipigana huko Mashariki ya Kati kwa takriban miaka 19. Huko Afghanistan na Iraq, takriban mashujaa wa jeshi letu 7,000 wamejitolea maisha yao. Zaidi ya Wamarekani 52,000 wamejeruhiwa katika vita hivyo. Tumetumia zaidi ya dola trilioni 7 huko Mashariki ya Kati.

"Hivi sasa tukiwa tunashirikiana na washirika wetu kuangamiza kikundi cha ISIS, ni wakati kuwapa mapokezi makubwa mashujaa wapiganaji wetu wanaorejea nyumbani.

"Kadhalika nimekuwa nikiharakisha mazungumzo ili kufikia maridhiano ya kisiasa huko Afghanistan. Majeshi yetu yamekuwa yakipigana kwa juhudi kubwa -- na tunawapongeza kwa ushujaa wao, hivi sasa tunaweza kuanza kutafuta suluhu ya kisiasa katika mgogoro huu wa muda mrefu uliouwa wengi."

"Kuhakikisha kuwa ufisadi wa kidikteta hautaweza kupata silaha za nyuklia, nimeiondoa Marekani kutoka katika makubaliano ya balaa kubwa ya nyuklia. Na kabla ya kuanza kipindi cha baridi tuliweka vikwazo dhidi ya Iran ambavyo havijawahi kuwekwa kwa nchi yoyote."
XS
SM
MD
LG