Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 17:06

Marekani: Trump kutoa hotuba kuhusu "Hali ya Taifa"


Rais wa Marekani Donald Trump Jumanne usiku anatarajiwa  kutoa hotuba yake yake ya pili ya hali ya kitaifa.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya mvutano kati ya White House na bunge kuhusu fedha za ujenzi wa ukuta na kupelekea kufungwa kwa baadhi ya idara za serikali kuu kwa muda mrefu Zaidi, katika historia ya Marekani.

Trump anatarajiwa kutoa hotuba hiyo mbele ya baraza la wawakilishi pamoja na Seneti.

Hotuba ya mwaka huu imekuja siku chache baada ya kufunguliwa tena kwa baadhi ya idara za serikali kuu, hatua iliyosababishwa na malumbano kati ya rais na baadhi ya wabunge kuhusu fedha za kujenga ukuta kwenye mpaka wa Mexico.

Kufungwa huko kulisababisha kuahirishwa kwa tarehe ya kulihutubia taifa.

Haya yanajiri huku tarehe iliyowekwa rasmi (Februari 15) ya kutatua mgogoro uliopo, ikikaribia.

Pande zote mbili -Wademokrat na Warepublican - zimekuwa zikijaribu kutafuta mwafaka kuhusiana na suala hilo huku baadhi ya wakosoaji wa Trump wakisema kwamba ni sharti kiongozi huyo alegeze msimamo aliouchukua ili kusuluhisha mzozo uliopo kuhusu sera za uhamiaji.

Trump ameashiria nia yake ya kuifunga tena serikali au kutoa amri ya kiutendaji na kutangaza hali ya hatari, ili kupata fedha za kugharamia ujenzi wa ukuta huo.

XS
SM
MD
LG