Wakazi wengi kwenye taifa hilo ambalo watu wengi hawajapokea chanjo. Chombo cha habari cha serikali kimesema kwamba makao makuu yanayofuatilia mambukizi ya virusi yameripoti visa vingine 269,510 vya maambukizi pamoja na vifo vya watu watatu. Idadi hiyo uyo ya vifo inafikisha jumla ya watu 58 wakati zaidi yaw engine milioni 1.48 wakisemekana kuambukizwa tangu mwishoni mwa Aprili nchini humo.
Rais mpya wa Korea kusini Yoon Suk Yeol amesema Jumatatu kwamba yupo tayari kusaidia Korea kaskazini kukabiliana na mlipuko wa Covid-19, iwapo Pyongyang itarithia. Kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un Jumapili aliitisha kikao cha tatu tangu Alhamisi wiki iliyopita , ili kujadili hali ya maambikizi inayoshuhudiwa. Ripoti zinasema kwamba wakati wa kikao hicho, Kim alilaumu maafisa wa afya kwa kuzembea katika kutoa matibabu pamoja na kuchelewesha upelekaji wa dawa.