Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:35

Ripoti : Inawezekana Korea Kaskazini inajiandaa kurusha makombora


Picha za satellite zikionyesha maeneo ya vituo vya kurushia makombora nchini Korea Kaskazini iliyokuwa ikionyeshwa katika televisheni ya Korea Kusini, Julai 24, 2018.
Picha za satellite zikionyesha maeneo ya vituo vya kurushia makombora nchini Korea Kaskazini iliyokuwa ikionyeshwa katika televisheni ya Korea Kusini, Julai 24, 2018.

Kuna kila dalili kwamba Korea Kaskazini inawezekana imeanza kutayarisha kurusha makombora angani, idhaa ya National Public Radio imeripoti.

Kituo hicho cha Marekani kimesema kuwa uchambuzi wa picha za satellite wa kituo cha Sanumdong karibu na Pyongyang unaonyesha harakati za malori, magari madogo, treni na vifaa vya ujenzi.

“Iwapo utaunganisha yote hayo yanayoendelea, inadhihirisha kuwa inalingana na pale Korea Kaskazini inapokuwa katika mchakato wa kutengeneza kombora,” amesema Jeffrey Lewis, mtafiti katika Chuo kinachotoa mafunzo ya Kimataifa cha Middlebury, California.

Lewis amefanya uchunguzi wa picha, zilizokuwa zimetumwa na DigitalGlobe, kampuni ya Kimarekani inayotoa huduma ya kusambaza picha za angani na ardhini.

Hatua hii mpya imekuja wakati Rais wa Marekani Donald Trump akisema atakuwa “amesikitishwa sana” iwapo Korea Kaskazini itaanza tena kufanya majaribio ya silaha za nyuklia baada ya mkutano wake wa hivi karibuni na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un.

Trump aliwaambia hayo waandishi wa habari Ijumaa wakati akijiandaa kusafiri kuelekea Alabama kushuhudia uharibu uliletwa na dharuba ya upepo mkali katika eneo hilo. Alisema kuwa kwa kiwango kikubwa ameweza kuboresha uhusiano kati ya Marekani na Korea Kaskazini hivi sasa akitumikia wadhifa wake wa urais.

“Angalia, nilipoingia madarakani,” amesema, “chini ya uongozi wa Obama, Korea Kaskazini ilikuwa ni balaa. Ilikuwa mnaelekea vitani, wananchi, iwapo mnajua hilo au hapana. … Nilikuwanimeachiwa matatizo.”

Aliendelea kusema, “ Hivi sasa hakuna tena majaribio ya nyuklia, hakuna chochote kile.

Lakini tusubirini tuone kitu gani kitatokea, lakini nitasikitishwa sana nikiona kuna majaribio ya nyuklia."

XS
SM
MD
LG