Zoezi la Jumatatu limehusisha kombora moja la Marekani na 7 ya Korea kusini yakilenga bahari ya mashariki inayojulikana pia kama bahari ya Japan. Jeshi la korea kusini limesema kwamba limerusha silaha hizo ili kuonyesha uwezo wake wa kujibu mashambulizi kutoka Korea kaskazini kwa njia ya haraka.
Jeshi la korea kusini limesema kwamba Jumapili lilifahamu kwamba Korea kaskazini ilifanya zoezi la kurusha silaha 8 za masafa mafupi kwa dakika 35, kutoka maeneo tofauti , pamoja na karibu kwenye mji mkuu wa Pyongyang. Zoezi hilo la urushaji silaha la Marekani na korea kusini ni la pili chini ya rais mpya wa taifa hilo Yoon Suk Yeol, ambaye ameapa kujibu vilivyo uchokozi kutoka Pyongyang.
Mei 25 Marekani na Seoul walifanya zoezi la pamoja na kurusha silaha, likiwa la kwanza tangu 2017 , pale Korea kaskazini iliporusha makombora matatu.