Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:23

Russia yaanza tena ushiriki wake katika makubaliano ya usafirishaji nafaka za Ukraine


Meli ya mizigo ya Rubymar, iliyobeba nafaka za Ukraine, inaonekana katika Black Sea karibu na Istanbul, Uturuki Novemba 2, 2022. REUTERS/Mehmet Emin Calsikan
Meli ya mizigo ya Rubymar, iliyobeba nafaka za Ukraine, inaonekana katika Black Sea karibu na Istanbul, Uturuki Novemba 2, 2022. REUTERS/Mehmet Emin Calsikan

Russia ilisema Jumatano inaanza tena ushiriki wake katika makubaliano ya kuwezesha usafirishaji wa nafaka za Ukraine kupitia Black Sea.

"Shirikisho la Russia linaona kuwa dhamana iliyopokelewa kwa sasa inaonekana ya kutosha, na kuanza tena utekelezaji wa makubaliano," wizara ya ulinzi ilisema katika taarifa.

Russia ilisitisha ushiriki wake Jumamosi baada ya kudai Ukraine ilitumia ndege zisizo na rubani kushambulia meli za Russia huko Black Sea.

Umoja wa Mataifa na Uturuki ziliafikiana na Russia na Ukraine ili kuanza tena usafirishaji wa nafaka wa Ukraine na kuruhusu usafirishaji wa mbolea kutoka Russia mwezi Julai huku kukiwa na mzozo wa chakula duniani.

Katika taarifa iliyotolewa Jumanne kupitia msemaji wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwa uchangamfu alikaribisha tangazo kutoka Shirikisho la Russia juu ya ushiriki wake tena katika Mpango wa Nafaka wa Black Sea.

XS
SM
MD
LG