Uhaba huo ni mbaya zaidi kuliko kilele cha vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 2013 na 2016, Shirika la Chakula na Kilimo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF na Mpango wa Chakula wa Umoja wa Mataifa (WFP) walisema.
“Kupungua kwa usalama wa chakula na kuenea kwa utapiamlo kunahusishwa na mchanganyiko wa migogoro, hali mbaya ya uchumi, hali mbaya ya hewa, na kuongezeka sana kwa gharama za chakula na mafuta," walisema katika taarifa.
"Wakati huo huo, kumekuwa na kupungua kwa ufadhili wa programu za kibinadamu licha ya kuongezeka kwa mahitaji hayo ya kibinadamu." Waliongeza.
Ongezeko la bei za vyakula duniani lililochochewa na uvamizi wa Russia nchini Ukraine, muuzaji mkubwa wa nafaka nje, kuliacha mashirika ya kibinadamu na upungufu wa fedha za wahisani.