Baraza hilo la Mawaziri kwa kawaida hujumuisha makamu wa rais na viongozi wa wizara 15 za utendaji, kama vile wizara za Mambo ya Nje na Hazina.
Pia linajumuisha takriban maafisa 10 watakaohudumu katika nafasi za ngazi ya baraza la mawaziri kama vile mwakilishi wa biashara wa Marekani, mkurugenzi wa upelelezi wa taifa na mkuu wa wafanyakazi wa White House.
Isipokuwa makamu wa rais na mkuu wafanyakazi, nafasi nyingine zote zinahitaji uthibitisho wa Seneti.