Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 07:17

Sudan : Jeshi, muungano wa demokrasia wasaini tamko la ushirikiano


Wananchi wa Sudan wakusanyika nje ya jela ya al-Huda mjini pacha wa Khartoum, Omdurman, Julai 4, 2019
Wananchi wa Sudan wakusanyika nje ya jela ya al-Huda mjini pacha wa Khartoum, Omdurman, Julai 4, 2019

Wawakilishi kutoka baraza la kijeshi la Sudan na muungano unaounga mkono demokrasia wamesaini tamko la kisiasa Jumatano ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya ushirikiano wa kuiongoza Sudan yaliyofikiwa mapema mwezi huu.

Sehemu nyingine ya mkataba huo, ni tamko la kikatiba, linalotarajiwa kusainiwa mapema Ijumaa.

Matokeo hayo ni hatua ya kusonga mbele katika siasa za mpito nchini Sudan ambapo kulikuwa na miezi kadhaa ya machafuko tangu jeshi kumpindua kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir.

Mkataba wa kushirikiana katika madaraka ni pamoja na kuundwa kwa baraza la kujitegemea la pamoja lililopewa jukumu la kuongoza nchi hiyo kwa miaka isiyopungua mitatu kabla ya uchaguzi mpya kufanyika.

Pande zote mbili pia zimekubaliana kuwepo uchunguzi huru juu ya vitendo vya jeshi kuwashambulia waandamanaji Juni 2019, ambapo waandaaji wa maandamano wanasema watu 128 walikufa huku wizara ya afya ikisema idadi ya waliokufa ilikuwa watu 61.

XS
SM
MD
LG