Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 06:04

Netanyahu akatisha ziara Marekani baada ya Hamas kushambulia Israeli


Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu anakutana na Rais wa Marekani Donald Trump Jumatatu, na bila ya kuchelewa ataanza safari yake kuelekea nyumbani, akatisha ziara yake ili aweze kushughulikia shambulizi la roketi lililorushwa kutoka Ukanda wa Gaza.

Netanyahu alikuwa amepangiwa kula chakula cha usiku White House, Alhamisi, na pia aihutubie Kamati ya Masuala ya Mahusiano ya Marekani na Israeli, kikundi kikuu kinachofanya ushawishi kwa niaba ya Taifa la Israeli.

Ameahidi katika tamko lake wakati akitangaza kufupisha ziara yake kwamba Israel itajibu shambulizi hilo kwa nguvu katika kile alichokiita ni “shambulizi la jinai” kwa Israeli.

Kombora hilo lilipiga nyumba katikati ya Israel, kaskazini mashariki ya Tel Aviv, na kujeruhi watu saba.

Jeshi la Israeli limekilaumu kikundi cha Hamas kwa kufanya shambulizi hilo na kusema itajibu shambulizi hilo kwa kuongeza nguvu zaidi za kijeshi katika mpaka wa Gaza.

Ziara iliyofupishwa ya Netanyahu imekuja wakati akitafuta nguvu ya kisiasa katika kinyang’anyiro cha mara ya pili, Aprili 9, na unaelekea kuwa ni uchaguzi mgumu kwake, na wakati Trump anatarajiwa kutambua rasmi haki ya Israeli kuendelea kukalia kwa mabavu eneo lenye utata la milima ya Golan Heights.

Israel ilikamata eneo hilo lilioko upande wa kaskazini mashariki ya Syria wakati wa vita ya mwaka 1967, iliyodumu kwa situ sita na baadae kuendelea kulikalia eneo hilo mwaka 1981.

XS
SM
MD
LG