Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:08

Wapalestina 15 wauwawa katika maandamano mpakani na Israeli


Mpalestina akitupa mawe kuelekea upande wa wanajeshi wa Israeli wakati wa mapambano kati ya waandamanaji wa Palestina na majeshi ya Israeli, huko ukanda wa Gaza Machi 30, 2018
Mpalestina akitupa mawe kuelekea upande wa wanajeshi wa Israeli wakati wa mapambano kati ya waandamanaji wa Palestina na majeshi ya Israeli, huko ukanda wa Gaza Machi 30, 2018

Wapalestina 15 wameuwawa na wengine zaidi ya 750 kujeruhiwa na majeshi ya Israeli Ijumaa wakati wakifanya maandamano kuelekea katika mpaka wa Israeli na eneo la ardhi ya Wapalestina la Gaza.

Hiyo ni siku ya maafa makubwa kuliko zote iliyoshuhudiwa huko Gaza tangu vita vya Israel na Hamas vilipozuka mpakani hapo mwaka 2014.

Siku ya Ijumaa ilikuwa ni mwanzo wa kile waandaaji wa maandamano hayo wa Hamas wamesema kutakuwa na maandamano ya kila siku yatakayodumu kwa wiki sita kupinga kizuizi kilichowekwa na Israeli mpakani hapo.

Walioandaa maandamano hayo wanasema yanakusudia kunyanyua sauti za madai ya Wapalestina ya “haki yao ya kurejea” kule ambako leo in Israel. Watu waliowengi ambao ni milioni 2 wanaoishi Gaza ni kizazi cha Wapalestina ambao walikimbia au kuondolewa kwa nguvu katika makazi yao mwaka 1948 wakati wa vita vya Mashariki ya kati vilivyopelekea kuundwa kwa taifa la Waisraeli.

“Haki hiyo ya kurejea” inadai kuwa ndugu wa wakimbizi ambao walipoteza makazi yao mwaka 1948 warejeshewe mali zao.

Jeshi la Israeli limewatuhumu wanamgambo wa Wapalestina kwa kutumia maandamano kuendesha mashambulizi ya siri.

Jeshi hilo limesema kuwa maelfu ya Wapalestina walikuwa wakitupa mawe na kuchoma matairi wakiyapeleka upande wa pili wa mpaka huo ambapo yapo majeshi ya Israeli.

Pia wameongeza kuwa katika tukio mmoja, Mpalestina mwenye silaha alipiga bunduki akiwalenga wanajeshi wa Israeli.

XS
SM
MD
LG